AZMA MPONDA WA ‘KIPIMO CHA PENZI’, DHAHABU MCHANGANI SEMA TU HAJASHTUKIWA,


Na Joseph Muhozi 'Josefly', Mtangazaji Victoria fm Musoma, Rapper

Kama Tanzania tunaweka kumbukumbu ya nyimbo zilizowahi kuhit ama zinazohit zaidi basi nyimbo za mapenzi zitachukuwa 75% kwa makadilio ya chini.
Lakini pia tukiangalia hata album za wasanii wanaoimba ambao ndio wanaongoza kwa kuimba nyimbo hizi basi wengi wao album zao zinabeba 90% love songs.
Lakini Sikuwahi kufikiria kama kuna Rapper (MC) wa TZ tena anaejiita ‘Hip Hop’ anaweza kurekodi album ama mixtape yenye nyimbo zote za mapenzi!! No, sikuwahi….nadhani wewe pia hukufikiria hilo, lakini AZMA ndiye aliweza kunibadili fikra baada ya kutangaza kutoa mixtape yenye nyimbo 15 ambazo zote ni za mapenzi.
Inawezekana kabisa jina ‘AZMA’ sio jina linalofahamika kwa watu wengi kama majina ya mastaa wengine, lakini naweza kusema katika uandishi na idea ‘ni dhahabu mchangani sema tu hajashtukiwa’.
Jina lake halisi ni AZMA MPONDA.Nilianza kumsikia AZMA nilipodownload wimbo wake unaoitwa ‘Bongo flava inakufa’, labda jina la wimbo na idea zilivuta zaidi kusikia imekuwaje. Mashairi yaliyokuwemo yana maneno makali kidogo akiwarushia bomu aliowaita bongo fleva na bongo fleva yenyewe, lakini alitoa sababu na mifano inayotoa picha ya kile kinachofanyika kweli, Ni wimbo unaofaa kukaa kwenye mixtape.
Hapo nikajikuta nakuwa mfuasi wa nyimbo zake taratibu na nikaunasa wimbo mwingine na kuudownload unaitwa ‘My name is Hip Hop’. Kiukweli nilipata ladha ya Hip Hop kweli na nikabaki na chorus kichwani “my name is Hip-, My father is Hop, I go by the name of Hip- Hop”.
Nikazidi kumfatilia taratibu kwa hili jina ‘AZMA MPONDA, UMABE’, nikamsikia kwenye nyimbo nyingine za watu kama ‘Saa mbovu’ aliyofanya na Nash Mc, Young Killer na Stereo, ‘Connection’ aliyofanya na Ezden na wengine na nyingine nyingi, baadae nikamsikia amejiunga na familia ya Tamaduni Music, nikaona hapo panamfaa huyu jamaa kwa sababu ni karakana ya Rhymes ataiva zaidi. Lakini  nikampigia salute tena nilipomuona kwenye Fid Friday Freestyle ya Mwanza nikakubali kweli ameiva.
Nakumbuka niliwahi kumualika mwaka jana kwenye show niliyokuwa naifaya Radio SAUT inayoitwa ‘HIP HOP 120’, na baada ya show nilimpigia salute kihip hop. Jamaa ni mkali.
Kwa jinsi nilivyokuwa namfahamu sikuwahi kuwaza kuwa ipo siku ntamsikia akiconcentrate kwenye love songs, lakini naweza kusema alinibadili mawazo na ndiye msanii pekee wa Hip Hop TZ niliyewahi kumsikia mimi amefanya album yenye nyimbo 15 zote za mapenzi, ama hata mixtape.
Kikubwa zaidi sio tu kutoa nyimbo nyingi za mapenzi, lakini kinachonishika zaidi ni uandishi wake wa hizo nyimbo za mapenzi.
Kipimo cha penzi ndio wimbo wa kwanza kutoka kwenye mixtape yake aliyoipa jina la LOVE STORIES.
Nilipousikiliza wimbo huu kwa mara ya kwanza tu niliurudia mara tatu, na hata nilipoucheza redioni (Victoria fm) wasikilizaji walikuwa wanatuma message wakiyarudia yale waliyoyasikia kwenye huu wimbo, na kuomba niucheze tena.
Kwa kweli huu ni utunzi ambao wasanii wengi inabidi kuuchukuwa kama mfano, ili kuishinda ile statement ‘kila siku mapenzi tu’, kwa sababu mapenzi yanatopic nyingi sana ambazo zinaweza kumfanya mtu ahisi anasikiliza ujumbe unaomhusu hata kama sio mfuasi wa mapenzi kiivo.
AZMA ameweza kuyazungumzia mapenzi kwa kujitoa yeye kabisa na sio kumuimbia girlfriend wake wala story ya mshikaji wake aliyetendwa, wala kuyalaumu mapenzi kwa sababu ya dhiki zake na kuachwa. Lakini ameweza kugusa angle tofauti tofauti kwa style ya kuuliza ni nini kipimo cha penzi? Na ukimsikiliza lazima utapata kitu cha kutafakari, kwa sababu kila kitu kimekuwa covered kwenye verse tatu ambazo zote hazilegilegi.
Ni kama anaongea na wewe, lakini pia ni kama anamwambia yule, wakati huo huo anaingia nae kidogo kwenye wimbo wake. Lakini kila angle anauliza hili swali nini kipimo cha penzi? Kweli Wengine wanalia, wengine wanacheka, na wanaocheka wanaweza kuwa waliaji watarajiwa and vise versa. So nini kipimo cha Penzi??
Mpangilio wa verse na mashairi mazito lakini mepesi kueleweka yanaweza kukupa picha ya maswali mengi yanayohusu mapenzi, na mikasa ya mapenzi na mwisho utajikuta unajiuliza ni nini kipimo cha penzi la kweli.
Ni vigumu sana kukosa mfano wako kwenye haya mashairi, hata kama sio direct basi kuna mstari utakugusa indirect.
Wimbo huu ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wengi hasa wa Hip Hop ambao wengi wao wanazichukulia poa nyimbo za mapenzi…lakini pia kwa waimbaji wanaoandika idea zinazofanana kila siku,…mapenzi yanaweza kuwa na uwanja mpana na yakahusisha mpaka siasa, historia, uchumi, afya, psychology, mazingira n.k. Yap hata mazingira, kama huamini basi soma kitabu cha DR.Msafiri, title nimesahau kidogo ila ni cha mazingira utaona jinsi mapenzi yakigeuzwa kuwa ngono yanavyoweza kuchafua mazingira, so hiyo pia ni idea.
Sasa kama ni hivi kweli unaweza kuona jinsi gani  mapenzi yakiandikiwa mashairi mazuri hayawezi kuisha wala kuboa hata kidogo, kwa sababu in every aspect of life mapenzi yamepenya.
Big Up sana AZMA MPONDA I really appreciate your work, na ambae hajakufahamu vizuri namualika aitafute na kuisikiliza hii mixtape ya LOVE STORIES.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates