Rihanna atumia jina la album yake kuwajibu walioiponda picha yake ya kwenye cover ya album hiyo.


Baada ya Rihanna kureveal cover ya studio album yake ya saba yenye jina “Unapologetic” watu wengi walitoa maoni kupitia mitandao ya kijamii kama facebook na twitter.
Album cover hiyo inayomuonesha Rihanna akiwa hajavaa chochote juu (naked), picha hiyo inaambatana na maandishi mengi kwenye mwili wake ambayo hayaeleweki japo mawili matatu yanaweza kusomeka lakini bado hayatoi picha inayoeleweka haraka. Kiasi cha kufanya fans wahisi labda ni majina ya nyimbo zitakazokuwa katika album yake, likiwemo jina ‘diamond’ na Unapologetic ambalo ndilo jina la album.
Katika picha ya album cover hiyo chuchu moja ya Rihanna imefunikwa na maandishi wakati nyingine ikiwa ameifunikwa na kiwiko chake cha mkono wa kushoto.
Watu wengi walitoa maoni mbalimbali baada ya kupata details za album hiyo ambayo inategemewa kuachiwa rasmi November 19, 2012 na wengi walionesha kusifia sana cover yake hasa ile picha na baadhi ya tweet za fans zilikuwa na maneno kama ‘I love that’, unapologetic sounds good‘ I’m so proud of her the cover and the name are totally Epic, Perfect, flawless etc’, na mengine mengi ya kusifia.
Lakini kuna walioponda na kushangaa hiyo cover iliyowekwa na wengine ikaonekana kama hii ni picha inayoonesha bad girl Rihanna ambae ni unapologetic.
Rihanna alionekana kutowajali ambao wameiponda na  aliamua kutumia maneno hayo hayo yaliyo kwenye cover la album akajibu critique za wasikilizaji kwa tweet “it's okay! Refer to: album title", akimaanisha she is unapologetic.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates