Chris Brown aweka wazi uhusiano wake na Rihanna, “ sitaki kuharakisha kitu, kuweka pete yeyote kwenye kidole cha mtu yeyote


The R&B star amefunguka vizuri zaidi kuhusu uhusiano wake na ex girlfriend wake Rihanna baada ya kuonekana pamoja mara kwa mara bila kutoa tamko rasmi linalozungumzia uhusiano wa wawili hao ukiacha mbali ile video aliyoiachia baada ya kuachana na Karrueche Tran na kukiri kuwa bado anawapenda wote.

The ‘don’t work me up’ hit maker amesema katika interview, “ni mimi kuwa mkweli na nafsi yangu. Mimi na Rihanna tuna historia, na mimi na yeye tutaendelea kuwa best friends, na tunafanyia kazi mahusiano yetu sasa.” Mkali huyo anajua kabisa kuwa watu wanasema mengi kuhusu mahusiano yao ambayo hayaeleweki vizuri mbele za watu, ni marafiki wa aina gani ama ni wapenzi wa aina gani hawa.

Kuhusu hilo akafunguka, “nadhani kila mtu anaguswa na hii situation ya zamani, bado ni hali ya hatari, kwa sababu ni yale tunayo-deal nayo leo na ndio maana nafanya Jenesse Center ambayo inaonesha kuwa domestic Violence sio sawa. Lakini kuhusu maisha yetu, nadhani watu wanatakiwa kuyapa nafasi, sio tu kuyapa nafasi, shut the hell up! Mwisho wa siku, maoni yoyote yale hayawezi kubadili chochote ninachofanya.”

Ingawa anafeeling kwa Rihanna, Breezy amesema haoni dalili za ndoa katika maisha yao ya hivi karibuni,na kwa nini aliamua kuachia video ambayo aliongelea kuhusu kuwapenda wanawake wawili.

“Ninapojisikia hali flani, iwe ni ya muziki ama emotion, najisikia ni vizuri kushare na watu, kwa sababu ni experience na fundisho katika maisha.”

Na kuhusu kuwepo na wazo la ndoa alifunguka, “sijaribu kuharakisha mambo, kuweka pete yeyote kwenye kidole cha mtu yeyote au kudanganya mtu yeyote. Ni bora niwe mkweli kabisa.
Angalia interview hiyo hapa:



Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates