Jarida la Bongo5 laingia mtaani.


Mabibi na mabwana, toleo  jipya la mwezi November la jarida ulipendalo la Bongo5 hatimaye limeingia mtaani rasmi likiwa na mastory kibao tena very exclusive. Mfahamu vizuri Salama Jabir kama ana mpenzi ama lah! Unafahamu kuwa anataka kuja kuwa mama siku moja? Nani wa kuziba pengo la Kanumba? Jipatie nakala yako kujua wadau wa filamu wanawataja akina nani! Kuna makala nyingine kama ‘Lulu na Kajala na mwisho unaosikitisha’, Feza Kessy aingia rasmi kwenye muziki, soma ujue alivyojipanga.
Kuna makala ya Swahili Rap Inspiration iliyoandikwa na Ezden Jumanne ambapo utafamu impact ya NikkiMbishi aka Baba Malcom, One the Incredible na Stereo kwenye Hip hop ya Tanzania.
Unataka kuwafahamu wasanii wa kiume wanaokimbiza zaidi sasa hivi Tanzania? Makala ya Bongo Kings itakupa jibu. Makala ya ujio wa Rick Ross waipa heshima Tanzania na wasanii watano waliofunika zaidi kwenye Fiesta. Makala ya Kona ya Mjasiriamali isemayo: ACHA KUTAFUTA KAZI, ANZA KUTAFUTA FURSA. Unawafahamu wanasayansi wachanga wa Tanzania?
Kijana unafahamu haki na wajibu wako? Pata nakala yako uzijue. Kuna safu inaitwa Haileweki ambapo kuna kali kama, Nani aliyemtupia TID skendo ya kutaka kumuua Ali Kiba? Pamoja picha za kuvutia za matukio kama Fiesta Dar, Uzinduzi wa filamu ya Skyfall - Mlimani City na mambo mengine mengi!!
Pata nakala yako kwa shilingi elfu tatu tu.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates