Major Harris wa “The Deflonics” Afariki dunia akiwa na miaka 65.

Anaitwa Major Harris…aliyekuwa member wa kundi la muziki wa soul kutoka Philadelphia “The Delfonics” ameripotiwa kufariki dunia huko Richmond, Virginia.
Vyombo vya habari vya karibu vimeripoti kifo hicho kutokea ijumaa Nov 09 kutokana matatizo ya moyo aliyokuwa nayo muda mrefu na kushindwa kufanya kazi kwa mapafu ambako kulipelekea kukimbizwa hospitali na baadae kufariki dunia.
Kihistoria Major Harris alianza muziki long time..mwishoni mwa miaka ya 50’s na aliwahi kuwa member wa makundi kibao tu kama Charmers, Frankie Lymon’s Teenagers na Nat Turner’s Rebeillion kabla hajamalizia muziki wake The Delfonics mwanzoni mwa 1970’s ambapo walitengeneza hits kama “La-La (Means I Love You) and “Didn’t I (Blow Your Mind This Time)”.
Wasanii kibao wa HipHop wa mid era wame-sample ngoma kibao za The Deflonics…baadhi yao ni pamoja na Grand Puba “Very Special”, Ghostface Killah “Holla” & “R.A.G.U.” na Fugees “Ready or Not”..R.I.P Major Harris.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates