Justin Timberlake na mkewe Jessica walikuja Tanzania kimyakimya Kwa ajili ya honeymoon na walifika Mara.


Ripoti toka United States ndo zinatufungua macho watanzania kuwa mwimbaji wa ‘what goes around comes around’ Justine Timberlake alikuja Tanzania na mkewe Jessica Biel kimya kimya kwa ajili ya Honeymoon a.k.a Fungate.
Wanandoa hao wapya walitua Kilimanjaro International airport October 21, na wakaelekea Singita Grumeti ambayo ni private reserve ndani ya hifadhi ya wanyama ya Serengeti ambayo iko mkoa wa Mara. Imesemekana kuwa wali-enjoy vilivyo uzuri wa Tanzania katika hifadhi ya wanyama pori na walizunguka sana kuona kila angle.
October 26 Justine Timberlake na mkewe walilala katika Faru-Faru lodges na Singita Grumeti, kabla hawajarudi tena Kilimanjaro airport October 30.
Inaonekana Jessica Biel ama Mrs. Timberlake anaizimia sana Tanzania na ameona ndio sehemu nzuri sana ya kula raha na kupumzika, kwa sababu hii siyo mara ya kwaza kwa mrembo huyo kuichagua Tanzania, January 2010 alikuja Tanzania na akapanda mlima Kilimanjaro akiwa na wasanii wengine kama Emile Hirch, Isabel I Lucas, Santigold, Lupe Fiasco, na wengine kibao na mission ilikuwa ni kukusanya mkwanja na kuongeza ufahamu wa watu katika tatizo la ukosefu wa maji safi linaloikumba dunia.
Justine Timberlake na Jessica Biel walifunga ndoa ijumaa October 19, huko kusini mwa Italy. Walionekana kufurahia sana ndoa yao mpya na kwa pamoja wakawaambia watu “it’s great to be married, the ceremony was beautiful and it was special to be surrounded by family and friends.”
Mr& Mrs. Timberlake naamini ilkuwa poa pia kuitembelea TZ na kucheki mazuri kibao tuliyopewa na Mungu na mtawambia na wengine kama Timberland waje nao sio kwa show tu hata kutembea na kula good time.

Kutokana na ujio wao wa kimya kimya haikuwa rahisi kwa waandishi wa habari kupata picha zao wakiwa Tanzania sababu hakuna aliyefahamu.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates