Nick Minaj azidi kukimbiza, Sikiliza hapa wimbo wake mpya ‘Freedom’


Kuprove kwamba yeye ni mkali hakuhitaji maneno bali vitendo, hiki ndicho rapper wa kike wa YMCMB ameonesha. Baada ya kuachia list ya track 27 zitakazokuwa kwenye album yake mpya Pink Friday:Roman Reloaded-The Re-Up, sasa ameachia ngoma moja toka kwenye album hiyo itakayokuwa na CD mbili na wakali kibao wamepewa shavu kuinogesha.
Fredom ndo jina la track hiyo na humo kweli kaonesha ukali sio kurap tu lakini hata kuimba pia anaweza.
Kwenye track hiyo Nick Minaj anajaribu kukumbuka enzi zake wakati anaanza kuingia katika ulimwengu wa muziki na kuwashukuru watu waliomsaidia kuvuka mambo kibao na kufika hapo alipo sasa. Lakini kama kawaida Rapper huyo wa kike hakuacha kuwachana wale ambao walikuwa wanajaribu kumrudisha nyuma ama kumchukulia poa.
“I feel free / I feel freedom / why they mad?/ You should see them. It’s crazy in her,” anafunguka Minaj kwenye chorus.
Minaj ametema mistari ya kujisifu kama kawaida tena kwa mitambao mizuri sana, “Freedom” ni ngoma ambayo inaonekana kupokelewa vizuri na fans wake na inatarajiwa kuanza kuchezwa kwenye vituo mbalimbali vya radio hasa hasa vipindi vya pop na hip hop.
“Pink Friday:Roman Reloaded-The Re-Up” itakuwa dukani na inaweza kununuliwa kwa kudownload kwenye iTunes.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates