H-Baba awashangaa mastaa wanaoomba chipukizi pesa kufanya collabo, anakuja na DVD ya show zake na 'Funga zipu'


Hamisi Baba a.k.a H-Baba amewashangaa wasanii wakubwa waliotoka wanaotangaza kuwa bila kulipwa kiasi flani cha pesa hawawezi kufanya wimbo wa kushirikishwa na wasanii chipukizi.
'Poteza hit maker' alifunguka katika interview aliyofanya na Josefly wa radio victoria fm baada ya kuulizwa yeye anahitaji kiasi gani kufanya collabo na msanii mchanga a.k.a chipukizzi.


"Hebu nambie msanii anakwambia eti kuimba na underground eti anataka hela! We muulize yeye wakati anataka kutoka nani alimuomba hela? Hivi huyo underground mwenyewe hela ya studio tu laki moja tu anakosa, halafu wewe unamuomba sijui millioni tano, anatoa wapi!?"
H-Baba alisema kwa kuwa bado yeye ni mkali wa stage, anataka kudhihirisha hilo kwa vitendo na hivi karibuni anatarajia kuachia DVD ya concert kibao alizopiga zikiwemo show alizopiga na wakali kama Koffi Olomide toka Congo.
Mkali huyo ambae anaaminika sana kwa kuja na idea 'unique' kwa ngoma anazoachia, amesema amejipanga kuachia ngoma yae mpya inayoitwa 'Funga Zipu' ambayo anaamini itauwa zawadi tosha kwa fans wake.
H-baba alitahadharisha kuwa TRA wawe makini wanapochukua pesa za wasanii wakati hawawezi kudhibiti wizi wa kazi za wasanii, na kwa kwamba ingebidi serikali ingetengeneza sheria ya kumlinda msanii kabla hawajawaza kuchukua pesa kutoka kwenye kazi zao. Akakazia "Wasanii wanahangaika kweli".

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates