Rick Ross anusurika kifo baada ya kukoswa na risasi 20! Hasimu wake 50 Cent asema kitu kuhusu tukio hilo

Big boss wa MayBach Music Group, Rick Ross amenusurika kupoteza uhai wake baada ya gari lake aina ya Rolls Royce kukoswakoswa na risasi kadhaa jana katika mitaa ya Laudedale Florida.

Rosay alikutana na tukio hilo baya wakati ikiwa ni birthday yake ambapo baada ya kusikia milio ya risasi iliyokuwa inaelekezwa kwenye gari lao, dereva wa gari hilo alijitahidi kukwepa na kuelekea upande ambao gari hilo lingekwepa risasi na mwisho kuuvamia ukuta wa jengo moja.
 Mashuhuda wa tukio hilo wameuambia mtandao wa aceshowbiz kuwa Rosay alikuwa na rafiki yake aitwae Moragne wakitoka Club LIV ya Miami alikofanyia birthday party yake ya kutimiza miaka 37.
Polisi wa jiji hilo walithibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini hakuna risasi hata moja iliyolitoboa gari hilo na wote waliokuwa kwenye gari hilo wako salama kabisa.
Bado haijajulikana nani ambae atakuwa amehusika na tukio hilo, Rosay aliwahi kupokea vitisho vya kuuawa wakati anapanga kufanya ziara yake, hata hivyo aliahirisha ziara hiyo japo alisema sio kwa sababu ya vitisho hivyo.
Rick Ross mwenyewe hajasema kitu kuhusiana na tukio hilo, lakini hasimu wake 50 Cent yeye anaamini kuwa hilo ni tukio la kujipangia tu. 50 Cent amepost kwenye Instagram picha ya gari la ajai hiyo na kuandika, "Hahaha fat boy hit the building? lol it looks stage to me. No hole's in da car."
50 Cent na Rick Ross wamekuwa hawaelewani tangu mwaka 2009.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates