JULIANA ASHINDWA KUJIZUIA

Juliana Kanyomozi, Diva ambaye anafanya poa sana kimuziki nchini Uganda ameonyeshwa kuguswa kwake na tukio la hivi karibuni huko Iganga Uganda, la mamlaka ya maji kusitisha huduma ya maji katika hospitali kwa miaka miwili sasa.



Kufuatia tukio hili ambalo lilifikia hatua ya kuzua maandamano ya wakazi wa eneo hilo yaliyoingiliwa na polisi, Juliana naye ameamua kutia sauti yake kuonyesha madhara ya hatua hii ya kusitisha huduma ya maji hospitali hususan kwa hospitali hiyo ambayo inahudumia watu wanaofikia 500 kwa siku.

Juliana ameungana na wananchi hawa pamoja na mbunge wao Mheshimiwa Peter Mugema kutaka mamlaka husika kurudisha huduma ya maji kwa hospitalini hapo, ili kuokoa maisha ya wengi, na kuangalia namna nyingine wanavyoweza kumaliza deni la shilingi milioni 30 za Uganda ambazo inadaiwa.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates