Banana katika kampeni nzito

Katika kupambana na wale watu ambao hutumia mitandao vibaya kutukana, kupotosha umma kwa habari za uongo tofauti na maadili yanavyokwenda, Msanii wa muziki Banana Zorro kwa pamoja na Mrisho Mpoto wameachia wimbo mpya unaoitwa  FUTA, DELETE, KABISA.


Wimbo huu ni kufuatia kampeni ambayo imeanzishwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA kuhamasisha matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii na mawasiliano.

Mkurugenzi wa TCRA , Prof John Nkoma amesema lengo kampeni hiyo ni kupunguza matusi katika mitandao ya kijamii na kupotosha jami kwa habari zisizokuwa na uhakika na za kuchochea vurugu.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates