MAMA MZAZI WA PROF JAY KUZIKWA JUMAPILI HII

Mama Mzazi wa wasanii wakongwe wa muziki wa kizazi kipya, Professa Jay na pia Black Rhino, marehemu Bi Rosemary Majanjara anatarajiwa kuzikwa Jumapili hii katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Taratibu za msiba wa mama huyu, zitaanzia asubuhi nyumbani kwa Professa Jay Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam kwa sala, na pia kutoa heshima za mwisho na kisha kuelekea makaburini katika maeneo ya maziko.

 

Wadau ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa staa wa rap hapa Bongo, Professa Jay, pamoja na ndugu yake Black Rhino, wameendelea kujitokeza kutoa pole pamoja na kushiriki kwa nafasi zao katika msiba mkubwa wa Mama Mzazi wa wasanii hawa ambao upo Mbezi jijini Dar es Salaam.

 

chiwileinc inaendelea kuwatakia wasanii hawa nguvu katika kipindi hiki kigumu, na Mungu ailaze roho ya amarehemu mahala pema peponi Aamin.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates