P Square watoa Msaada kwa producer OBJ

P Square ambayo inaundwa na wasanii wakali,  Peter pamoja na Paul Okoye kutoka nchini Naijeria, Wametoa kiasi cha

 shilingi milioni 40 kama sehemu ya mchango wao kusaidia matibabu ya Mtayarishaji mahiri wa muziki nchini humo, OJB Jezreel ambaye amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya Figo.

Mtayarishaji huyu mahiri, kwa sasa yupo katika mishe za kuchanga fedha kwaajili ya kufanikisha zoezi la kubadilisha figo, ambapo pia wasanii wengine kama vile Iyanya, Ruggedman, Don Jazzy, Dele Momodu, Mercy Johnson Julius Agwu na wengineo wamekwishashiriki kumsaidia OJB.

Kitu ambacho kimewagusa wengi kutoka katika hatua hii ya P-Square, ni kitendo cha wao kuonyesha utayari na moyo katika kumsaidia licha ya kuwa hawakuwahi kufanya naye kazi hata kidogo ambayo pengine ingekuwa imewawekea ukaribu.

 

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates