Rabbit makini na maisha

Rabbit aka Kaka Sungura, rapa ambaye anafanya poa hivi sasa katika chati za muziki mbalimbali Afrika Mashariki kutoka ngoma yake ya Ligi Soo, ametajwa kama mfano mzuri wa kuigwa kutokana na jitihada zake zilizomtoa katika maisha ya chini kabisa na hali duni mpaka kufikia ngazi hii ya Ligi Soo.
 
Historia ya msanii huyu inaanzia kwenye maisha duni na uhaba wa fedha ambao ulisababisha yeye kusoma kwa tabu na kufanya biashara za hapa na pale kabla ya kuingia katika muziki ambapo alianza kama 'backup singer' wa rapa Chiwawa.
 
Historia hii yenye mafunzo mengi ya rapa huyu, ni moja kati ya udhibitisho tosha kwa kila mtu ambaye anajaribu kutumia uwezo wake kufanya kile anachokipenda kuwa, wakati wote ukijituma mafanikio lazima yatakufuata

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates