Sehemu ya stori kubwa za AMPLIFAYA ya @CloudsFM mwaka 2012
ilikamilishwa pia na ripoti za staa wa Kenya CMB Prezzo kukutana na Jay
Z, baada ya ushindi kwenye nafasi ya pili kwenye jumba la Big Brother
Africa 2012, Prezzo alipata dili la One Campaign ambalo pia Jay Z ni
mmoja wa mastaa waliopewa shavu kama hilo.
Siku kadhaa baadae Prezzo alisafiri mpaka Marekani ikiwa ni sehemu ya
majukumu ya One Campaign ambapo pia alikutana na Jay Z kwenye jiji la
New York.
Sekunde zako 26 unaweza kuzitumia hapo chini kutazama hii video ya
Prezzo alipokutana na Jay Z, rapper ambae ni mmoja wa mastaa wa dunia
ambao sio rahisi kumfikia hata kupata picha pamoja nae, rapper ambae
hata kujibu tweets huwa ni ngumu sana…. juzijuzi alijibu tweets kwa mara
ya kwanza ikawa ni historia na nilimsikia Dee Andy wa XXL Clouds FM
akiripoti kwenye 255 kwamba twitter wenyewe ilibidi wampigie simu
kuuliza kama ni yeye kweli au kuna mtu kaingia kwa kuibia?
Home »Unlabelled » STORY YA JAY Z KUKUTANA NA PREZZO CHECK VIDEO HAPO CHINI
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment