Juhudu za uokozi zimeanza tena Kusini mwa Utaliano baada ya boti iliyokuwa imewabeba wahamiaji wa kiafrika kwenda Italia, kuzama katika kisiwa cha Lampedusa.

Baadhi ya waliopoteza maisha yao wakitafuta kuingia Ulaya

Boti hiyo ilizama ikiwa imesalia na kilomita moja kufika katika ufuo wa bahari siku ya Alhamisi.
Hadi sasa miili 113 imepatikana wakati kati ya waliokuwa katika boti hiyo miambili wakiwa hawajulikani waliko.
Kwa mujibu wa maafisa wa uokozi, idadi kubwa ya miili ya wahamiaji hao inaaminika kuwa ndani ya boti hiyo iliyozama.
Zaidi ya watu 150 waliokolewa. Wengi wa waliokuwa katika boti hiyo waliwa raia wa Somalia na Eritrea wakiwa katika safari ya kutafuta hifadhi nchini Utaliana. Inaaminika boti hiyo ilikuwa imewabeba watu 500
Kwa mujibu wa taarifa za serikali ya Utaliana ,mmiliki wa boti hiyo ambaye ni raia wa Tunisia alikamatwa
Aliwahi kufukuzwa kutoka nchini humu mnamo mwezi Aprili.
"Huu sio mkasa wa Italia, ni mkasa wa Ulaya na sharti kisiwa cha Lampedusa kionekana kuwa kitovu cha kuingilia Ulaya wala sio Utaliana tu,'' alinukuliwa akisema afisaa mmoja wa serikali .
Kote nchini Utaliana, kutakuwa na kimya cha dakika moja kuwakumbuka walioangamia.
kwa sababu ya kutokuwa na stakabadhi zinazohitajika, njia pekee ya wahamiaji wa kiafrika kufika Ulaya ni kupitia baharini kwa kusaidiwa na makundi ya wahalifu.
Mwandishi wa BBC Allan Johnston anasema kuwa wakati huu ambapo,mawimbi ya bahari ya Mediterranea yanakuwa yametulia, mamia ya wahamiaji huwasili katika fuo za kisiwa hicho karibu kila siku.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates