Ameniacha na Kumfata Mwanamke Mwengine Mpya; Nifanyeje Aweze Kunirudishia Pesa Nilizomkopesha...?

Mwanamke huyu alikuwa akimpa hela mpenzi wake akitegemea kuwa angekuja kumuoa, ila mambo yakawa ndivyo sivyo....

HII NDIO STORI KAMILI

Tulikuwa na mpenzi wangu kwenye mahusiano kwa miaka mitatu na mpango wetu ilikuwa ni kufunga ndoa. Mwaka jana mwezi April alinichumbia ila kutokana na mambo ya kifamilia harusi yetu ilishindikana mwezi kama huu mwaka jana yaani November 2012. Licha ya kuvunjika kwa uchumba wetu, ila tulikuwa tukionana mara kadhaa mpaka tulipokuja kuachana rasmi mwezi August mwaka huu.

Mwanzoni nilikuwa na imani kwamba labda tungeweza kuyamaliza matatizo yetu na kusonga mbele na mipango ya ndoa ila haikutokea hivyo. Na sasa hapa ndipo kwenye tatizo...

Mwaka jana tukiwa kwenye penzi moto moto nilimpa aliyekuwa mpenzi wangu kiasi cha sh. millioni 5 kwa ajili ya mradi aliokuwa akijihusisha nao. Nilimkopesha hizo hela sababu niliamini angekuja kuwa mume wangu na kama biashara ingefanikiwa ingeweza kutusaidia wote wawili.

Ila mara baada ya kutengana na akiwa yupo na mahusiano mengine kiukweli nazihitaji hela zangu. Nimekuwa nikimuuliza kwa miezi miwili iliyopita na amekuwa akinijibu utumbo huku akiwa hapokei simu yangu.

Kiukweli biashara anayoifanya inaonekana kufanya vizuri na amekuwa akiingiza hela kwa sana.

Je ni sahihi kwa mwanamke mwengine kufarahia matunda ya jasho langu? Nazihitaji hela zangu, nifanyeje niweze kuzipata...?

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates