LINEX AKABIDHIWA MTOTO WAKE MWENYE MIAKA MI 8

Hitmaker wa Kimugina Linex Sunday amesema amekabidhiwa mtoto wake ‘Richard Sunday’ kutoka kwa mpenzi wake ambaye alimficha kutokana usalama wa Linex wakati wa mahusiano yao.
3b4f310c4d4c11e3b003124d21716300_8


Akizungumza , Linex alisema alikuwa hatambui kama ana mtoto mwenye umri wa miaka nane kwakuwa alifichwa na mpenzi wake kutokana na mambo ya kifamilia kati ya wapenzi hao wawili.
“Kweli nimefurahi sana kupata kitu ambacho haukukitegema. Kwa sasa nimetoka kumchukua katika shule ambayo alikuwa anasoma nataka kumhamisha,” amesema Linex
“Unajua mambo ya wanaume jinsi tulivyo,mimi nimeshindwa kuruka kwasababu kitu alicho kifanya ni cha kijasiri sana.”

e4d51a304dcd11e3a326128d1742166d_8  
Mtoto wa Linex Sunday,Richard Sunday
Hata hivyo Linex amesema hataki kusema nini kilitokea kati yake na mzazi mwenzake kwakuwa anaandaa documentary ya tukio hilo itakayokuwa na mambo mengi excusive kuhusu yeye na mahusiano yake pamoja na mtoto itayotoka wiki ijayo na kuisambaza kwenye TV mbalimbali.

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates