SERIKALI YA JAMHURI YAOMBWA KUISADIA ZANZIBAR KATIKA WAZO LAKE LA UNUNUZI WA MELI KUBWA YA MIZIGO NA ABIRIA.



Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeshauriwa kuungana na Serikali ya Zanzibar katika nia yake ya kununua meli kubwa kwa ajili ya mizigo na abiria ili kutoa huduma bora ya usafiri kati ya Dar es Salaam, Zanzibar na Pemba na kuepusha ajali za mara kwa mara.
 Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mipango na Sera wa Chama cha Wakulima Tanzania 
 
Kanda ya Zanzibar Bw. Rashid Yusufu Mchenga, ambapo amesema kuwa, pamoja na nia nzuri ya Serikali ya Mapinduzi ya kununua meli kama huku ikijibana kibajeti kwa kiasi kikubwa.
 Bw. Mchenga amesema maafa yaliyotokea kwa siku za hivi karibuni kutokana na kuzama kwa meli kubwa tatu za abiri za Mv. FATIHI,  Mv. SPAICE SLANDER na MV SKAGIT inatokana na Serikali yenyewe kutokuwa na meli ya uhakika.
 Amesema kuwa matokeo ya ajali hizo yamewagusa karibu Watanzania wote na hivyo ukimya ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika suala la ununuzi wa meli kubwa ya Serikali ya mizigo na abiria haileti picha nzuri kwa wananchi wake wanaotegemea usafiri wa majini kwao pamoja na mali zao.
 ”Tumechoka kuona ama kusikia Watanzania wanapoteza maisha na mali zao kwa uzembe unaoweza kuepukika”. Alisema Bw. Mchenga.
 Amesema kuwa katika kifungu namba 14 cha katiba ya Muungano kinaelezea wazi kabisa juu ya haki ya kuishi na hivyo ajali za mara kwa mara zinazokatiza maisha ya Watanzania wenzetu, ni kinyume na sheria hiyo.
 Bw. Mchenga amesema kama ilivyo katika kuimarisha huduma ya usafiri wa treni za abiria na mizogo kwa mikoa ya Tanzania bara, pia kuna haja Serikali  kuona uwezekano wa makusudi wa kuimarisha usafiri wa abiria na mizigo majini kwa maana ya bahari, maziwa na mito.
 Amesema usafiri kwenye Maziwa kama Viktoria, Tanganyika, Nyasa na katika vivuko kwenye mito mikubwa kama Kirombero, Wami, Kagera, Pangani na Ruvu unaweza kukumbwa na tatizo kama vivuko na madara hayo hayataangaliwa kwa ukaribu.
 Ametilia mfano meli ya Mv. Liemba inayosafarisha abiiria na mizigo kwenye ziwa Tanganyika wanaofanya safari kati ya Kigoma nchini Tanzania na Buurundi kwamba imepitwa na wakati na kuna haja ya Serikali kuona umuhimu wa kutafuta meli nyingine ili maisha ya wasafiri kwenye eneo hilo  yawe ya uhakika.
“Mimi naona kuna haja ya Serikali kujitathimini na  kujipanga upya kwa kuangalia vipaumbele na kuimarisha vikosi vyetu vya uokoaji ili kusaidia kazi za uokozi zitokeapo ajali.” Alisema Bw. Mchenga.


Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates