HUZUNI: Raisi wa Zamani wa Afrika Kusini ndugu NELSON MANDELA AMEFARIKI DUNIA jana baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Raisi wa zamamni wa Afrika ya kusini bwana Nelson Mandela amefariki dunia jana jioni akiwa na miaka 95 baada ya kuugua na luzwa kwa muda mrefu hospitalini alipokuwa akipatiwa matibabu.


Taarifa rasmi toka serikali ya Afrika kusini zimethibitisha kifo hicho cha ndugu Mandela na tayari raisi wa Afrika kusini mr. Jacob Zuma ametuma salamu za rambirambi kwa familia na wanachi wote wa afrika ya kusini na duniani kwa ujumla walioguswa na kifo hiki.

Mandela atakumbukwa kama mfano na alama ya Afrika kwa kuongoza mapambano makubwa dhidi ya ubaguzi wa Rangi nchini Afrika kusini na Afrika kwa ujumla.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen
 

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates