PICHA - WANAUME WA JAPANI WAMESOMA KOZI HII ILI KUVUTIA WANAWAKE

Najua kuna watu wangu ambao sasa wapo kwenye mchakato wa kuoa au ndio wanatafuta mtu ambaye wataishi nao, lakini inawezekana kumekuwa na changamoto, Sasa leo September 20 2016 nakusogezea hii inayotokea nchini Japan ambapo wanaume ambao bado hawajaoa wanahudhuria kozi ya kulea watoto ili kumvutia mwanamke zaidi.

Bachelor hao wa kijapan wamehudhuria kozi ya kulea watoto ili kuongeza nafasi ya wao kupata wapenzi, Mwalimu wa kozi hiyo Takeshi Akiyama amesema lengo la kozi hiyo ambayo imeandaliwa na Ikumen University ni ili kusaidia mtu ambaye hajaoa kupata mke.

Masaya Kurita (31) bachelor anayeishi Tokyo Japan ameanza kozi baada ya kutafuta mke kwa miezi sita iliyopita, Aidha anaamini kuwa kufanya mazoezi ya kulea mtoto kwa kutumia plastiki kunaboresha nafasi yake ya  yeye kukukbalika kwa mpenzi .

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates