NEWS - MTEMVU ASHINDWA KESI YA UBUNGE TEMEKE

Aliyekuwa Mbunge wa Temeke (CCM) Abbas Mtemvu, ameshindwa kesi ya uchaguzi dhidi ya Abdallah Mtolea(CUF) aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana.

Mtemvu aliyekuwa akitetea kiti hicho katika uchaguzi Mkuu wa mwaka jana alifungua kesi  katika  Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akipinga matokeo yaliyompa ushindi  Mtolea.
Pamoja na mambo mengine akidai kuwa kura  za baadhi ya vituo vya kupigia kura hazikujumlishwa katika matokeo ya jumla.

Hata hivyo Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa   na Jaji Issa Maige aliyekuwa akisiliza kesi hiyo imetupilia mbali madai ya Mtemvu na badala yake imemthibitisha Mtolea kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.

Katika hukumu hiyo Jaji Maige amesema kuwa Mtemvu ameshindwa kuthibitisha madai yake jinsi yalivyoathiri ushindi wa mbunge huyo, huku akisema kwamba kasoro alizokuwa akizilalamikia Mtemvu hakuathiri ushindi wa mbunge huyo.

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates