WATOTO YATIMA WAENDA UTURUKI

Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad leo amekutana na uongozi wa Jumuiya ya Muzdalifat inayoyojishughulisha na utunzaji wa mayatima, pamoja na watoto wanaotarajia kusafiri kuelekea nchini Uturuki. Mwenyekiti wa jumuiya hiyo sheikh Abdallah Hadhir Abdallah amesema watoto hao wanne wanakwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kushiriki katika kongamano la kimatifa kuhusu maadhimisho ya siku ya watoto yatima linalotarajiwa kufanyika mjini Istambul Uturuki kuanzia tarehe 28 mwezi huu hadi tarehe 3 mwezi ujao.
Watoto hao Salum Ali Mohd (miaka 10), Hajir Khalid Haji (miaka 11), Shufaa Mohd Ali (miaka 12) na Lutfia Sheha Mussa (miaka 11) wataongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Muzdalifat Sheikh Abdalla Hadhir, Katibu wa Jumuiya ustadh Farouq Hamad Khamis na Mkuu wa kitengo cha mayatima Zanzibar Nassra Suleiman Abdallah.
Mapema Maalim Seif aliwakabidhi watoto hao bendera ya Zanzibar na kuwataka kuiwakilishi vyema nchi yao. Watoto hao na viongozi wao wanatarajiwa kuondoka nchini tarehe 28 mwezi huu.
lofanyika mjini Istambul Uturuki kuanzia tarehe 28/05 hadi 03/06/2012

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates