Home
»Unlabelled
» AFANDE SELE ATOA TAMKO KUTOKANA NA FUJO ILIYOTOKEA ZANZIBAR MUSIC AWARDS
AFANDE SELE ATOA TAMKO KUTOKANA NA FUJO ILIYOTOKEA ZANZIBAR MUSIC AWARDS
By
Unknown
•
1:07 PM
•
•
Mfalme
sele ameamua kufunguka baada ya kukaa kimnya sana tangu siku ya tukio
la zanzibar music awards ambalo walishindwa kupafom yeye na swahihiba
yake 20percety na kusababisha fujo iliyo dumu kwa takribani nusu saa
bwawani hotel na baadae kuhamia kituo cha police malindi.
Leo kwenye ukurasa wake wa FACEBOOK amefunguka kama ifuatavyo tembea nayo....!!!!!
Salaam Ndugu zangu wote mashabiki na wadau wa muziki wetu!!
Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na Twent Percent kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award.
"Tulialikwa kwenye ZANZIBAR MUSIC AWARD, na kabla ya kazi makubaliano
yote ya kazi kwa mujibu wa mkataba yalifuatwa, makubaliano hayo
yalihusisha sisi kujigharamia gharama zote za nauli na Malazi
(accomodation).
Tulifika Zanzibar salama,
tulipokua Zanzibar twenty alitaka agharamiwe huduma zote ambazo ni nje
ya mkataba wetu, nikamuomba na kumsihi sana Ndugu yangu aheshimu
mkataba, asitafute matatizo kwani tayari mpaka wakati huu tuna kesi na
Halmashauri ya Manispaa ya Moro ambayo kimsingi sikuhusika (nilishatolea
ufafanuzi siku za nyuma).
Lakini yeye alipingana na mimi,
akanibishia na kunisukuma Mbele ya.......... wageni na wenyeji wetu, wakiwemo
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiph Ali Idi, Waziri Seiph
Khatibu.
Walikuwepo waadishi wa habari wa siku Nyingi Akiwemo
Abubakari Liongo (idhaa ya kiswahili radio Ujerumani), Mkurugenzi wa
ZENJI FM ndugu Tua Saidi Tua.
Mimi Selemani Abdallah Juma Msindi
sihusiki kwa namna yoyote, na tabia zisizo za kuridhisha zinazoonyeshwa
na Ndugu yangu Twenty Percent, ambae nimekua nae nyumbani kwangu hata
kabla ya Tuzo zake Tano (Kili Music Award) ambazo kazi hizo zote hizo
kaandikia nyumbani kwangu siwezi kuwa na tatizo nae ni ndugu yangu
kiimani na kikazi, hata kazi yangu niliyofanya nae kabla siku za nyuma
"MBELE YAKO NYUMA YANGU" .. Kuna mstari Nilisema " ..Kuandika Rhyme
kwenda Gym kimtindo kuonyesha Ugum, bado unatakiwa uwe na nidhamu ya
kweli, sio ya kumzuga Mwalimu, utajihukumu".
Nimekua nikisisitiza
nidhamu kwa Ndugu zangu woote toka enzi za Ghetto BoyZ, Watupori na
Mabwasha'Kingdom, ambao wengine hawafanyi sanaa, ila nipo nao kwenye
Familia yetu kubwa hapa Tanzania. Nimesikitishwa na kitendo hicho. Siku
zote nimekua mwenye kuhitaji suluhu kwa namna ya Amani.
Verry sorry
kwa wote ambao mumefadhaika kwa hilo. Tuendelee kuwa pamoja na msisite
kutoa ushauri wenu, maoni ili Game letu lisonge. MUNGU ATUBARIKI.
Asanteni sana.
Selemani Juma Abdallah Mutabhazi Msindi.
a.k.a Afande Sele (King of Rhymes)
SIMILAR ARTICLES
Post a Comment