Kufuatia maswali mengi ya mashabiki wa
muziki kuhusiana na kinachoendelea baada ya Msanii Linex hapo awali
kutangaza kufanya kolabo na msanii mkubwa wa Uganda Keko, jambo ambalo
halijafanyika, Linex ameongea na eNewz kufafanua juu ya mchongo huu.
Linex ameweka wazi kuwa, ratiba ya kwake pamoja na ya Keko ambazo
zimekuwa na mambo mengi ndiyo kikwazo kikubwa ambacho kimefanya mchongo
huu kuwa haujakamilika mpaka hivi sasa.
Msanii huyu ameeleza zaidi kuwa, Amekwishafanya jitihada za mara
kwa mara kuwasiliana na Keko kumuuliza amefikia wapi na kukamilisha
kipande chake kilichobakia ambapo kutokana na mambo mengi, Msanii huyu
kutoka Uganda bado hajaweza kufanya kipande chake.
Linex amesema kuwa kwa sasa ameamua kutulia hadi msanii huyu wa
Uganda atakapoamua kumalizia sehemu yake mwenyewe kwasababu kolabo hii
inaumuhimu kwa pande zote mbili kwa kuwa yeye kama Linex ni msanii
mkubwa hapa Tanzania, na Keko ni mkubwa kwa upande wa Uganda.
Post a Comment