Maisha Plus 2012 yaendelea na usaili

Kaka Bonda, Kipanya na Mwanahamisi wakiwa redioni

Baada ya kukamilisha usaili Dodoma, Kahama, Kagera,Singida, Mwanza, Morogoro, Iringa sasa usaili unaelekea mkoani Mbeya ambapo utafanyika Sept 15 .

Crew nzima ya Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula inayodhaminiwa na banki ya NMB na Oxfam  baada ya hapo itaendelea na safari kutoka Mbeya moja kwa moja mpaka Kilwa, ambapo itafanya usaili  Septemba 17, kesho yake yaani Septemba 18 usaili utaelekea Masasi  mkoani Mtwara.

Dada Mwanahamisi akiongea na vijana
Septemba 20 itakuwa zamu ya Wanzanzibar kusailiwa katika kumpata mwakilishi wa Maisha Plus  kisha timu itarejea Dar tayari kwa usaili ambao utafanyika Septemba 22 na 23.

Kitakachofuata baada ya usaili wa Dar ni kipindi cha Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula kuanza kuonekana kwenye runinga yako. Usikae mbali na TBC1 kwasababu ndiyo itakayokusafirisha  nchi nzima ukiwa kwenye sofa lako nyumbani.
Team iliyojitolea kuingia msituni kutafuta vijana watakaoingia kijijini
Kubwa kuliko
Wakati usaili ukiendelea mikoani hapa nchini, Huko nchini Burundi nako usaili wa kuwapata washiriki wawili ulikuwa unafanyika kwa maana hiyo safari hii shindano la Maisha Plus litakuwa na washiriki kutoka huko.
Huu ni mwanzo wa shindano hili wa kuzishirikisha nchi zote za Ukanda wa Mashariki ya Afrika.

Kwa wakazi wa Dar fomu za ushiriki zinapatikana katika duka la Masoud Kipanya lililopo Millenium Tower,  Kijitionyama. Unaweza kupata usaidizi ka kupiga namba hii  0717 710303.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates