Dogo Janja ana mpinzani mpya. Bahati mbaya ama nzuri sio
member wa Tip Top Connection. Anaitwa Dogo Tundu wa Arusha. Amini usiamini, dogo ni mkali
balaa. Huenda ni maarufu jijini Arusha lakini kwenye cypher hii ya Wanene
huenda akatambulika rasmi nchini.
Kwenye cypher hii, wakubwa wamemwacha amalize verse
ya mwisho na kuonesha ujuzi mkubwa kwenye punch na mashairi makali kama:
“Naitwa Dogo Tundu, rap sio mzungu, usiniletee kiwingu,
nitakupiga manundu
Mimi ni kirusi nipo fast, kasi kama risasi kwenye beat
nawapiga nazidi kukunja ngita,na siwezi kucheka hili life nimeteseka, machizi wameweka
ngita kamanda bado napita mbuga nachapa kama mjeda, nimesimama imara kama Slaa
wa Chadema.”
Lakini Dogo Tundu hakuishia hapo akaamua kumchana Dogo
Janja:
“Nimezaliwa R, sijazaliwa Dar, mimi sio mshamba kama Janjaro
wa Dar
Hakuna Dogo Janja, wala Dogo Jinga , yeye ni sharobaro
na mimi ni mniga
Akitema Kirangi mimi nachana hadi Kichaga
Anaiga ushoga eti yeye ndo sharobaro.”
Post a Comment