Amber Rose ambae ni girlfriend wa Rapper
Wiz Khalifa ameandika tweet kwa followers wake million 1.4 iliyotaja jinsia ya
mtoto wao wanaemtarajia. lakini katika
tweet hiyo anaonesha kama hakuwa na plan ya kutaja jinsia ya mtoto huyo ila ni
kama ameitaja accidentally,wanatarajia mtoto wa kiume.
Lakini hii inawezekana aliamua tu kwa
sababu ameandika katika tweet moja hiyo hiyo message inayotaja jinsia ya mtoto
wao mtarajiwa na hapo hapo anashtuka kama kataja bila kujua.
Tweet yake ya jumapili ilikuwa inasomeka
“My friend Maria bought our Lil Boy this Slash onesie….Oops did I say Lil
Boy???
Hata hivyo Media za U.S.A zimefatilia sana
kujua jinsia ya mtoto mtarajiwa wa mastaa hawa, na wiki iliyopita gossip sites
zilitangaza jinsia ya mtoto wao na kusisitiza kuwa wamefatilia na wamepata
uhakika kuwa ni mtoto wa kiume na hii ni kutokana na shopping wanazofanya
mastaa hawa ambapo vitu vinavyonunuliwa kwa ajili ya maandalizi ya mtoto wao
inaonesha wazi kuwa ni mtoto wa kiume, hasa vitu vya rangi ya blue.
Lakini hata ukifatilia statement za Wiz
Khalifa mwenyewe huwa anataja kiwakilishi ‘HE’ akiwa anamzungumzia mtoto wao
japo hajawahi kusema kuwa ni mtoto wa kiume lakini hii pia ilikuwa inamaana.
Mwezi August alimwambia rapper Colloway “You’re going to teach him how to rap.”
Hivi karibuni pia Amber Rose alipokuwa
anazungumzia mipango yao ya kumpokea mtoto wao katika maisha yao alisema
wanapanga kuoana kwanza kabla hajajifungua mtoto.
“Nah, hakuna tarehe iliyopangwa bado.
Lakini tunaweza kupata license na kufunga ndoa kabla mtoto hajazaliwa, na
tutafanya sherehe baadae kwa sababu italeta maana kwa mtoto kuzaliwa katika
wedding na zaidi ya kuwa katika hii hali ya ujauzito tu. Watu wengine
wanaharakisha na kufanya. Lakini njia zote zinawezekana” alisema Amber Rose ambae
ni Ex girlfriend wa Kanye aliyezama kwenye bahari ya penzi la rapper Wiz
Khalifa.
Post a Comment