Afsa |
Ingawa Ney wa mitego ni jina ambalo wengi
tunaamini kabisa halikubaliki kwa baadhi ya
wasanii wa bongo movie hasa wasichana baada ya kutoa wimbo wake ‘Nasema
Nao’, na kufikia hatua ya kurushiwa maneno makali na baadhi ya waigizaji wa
kike TZ, Afsa Omary Neema 20% yeye sio
tu kuwa anamzimia Ney wa mitego, lakini anataka awe mmewe wa ndoa kabisa and
that’s that.
Kwa mujibu wa blog ya wajanja club katikati
ya mwezi huu, Afsa Omary a.k.a Neema 20% kwa kinywa chake alifunguka, “Si siri
nampenda sana Ney wa Mitego na natamani awe mume wangu wa ndoa hata kesho kama
akikubali, kama ingekuwa wasichana tunaruhusiwa kuwatongoza wanaume na kuolewa
nao basi mimi ningekuwa wa kwanza kwa Ney, ana mvuto na shababi.”
Sifa hazikuishia hapo, Afsa Omary a.k.a
Neema 20 alidai kuwa anampenda mwanaume anaejiamini na mtanashati na muonekano
anaouona kwa Ney wa Mitego na sio mtu mwingine na atafanya kila juhudi aweze
kuishi na msanii huyo ambae kila akitoa wimbo lazima ulete gumzo.
Afsa Omary, Neema 20% kama wanavyomuita ni
muigizaji aliyeibuka kupitia filamu ‘Furaha Iko wapi’ iliyotungwa na msanii wa
bongo fleva Hamisi Kinzasa a.k.a 20 percent.
Habari ndiyo hiyo, ukweli anao mwanadada
huyu mwenyewe kwa sababu hisia za mtu hazionekani tungepima tuhakikishe.
Post a Comment