C9 ATOA POSA KIJIJINI KWAO

Producer C9 Atoa Posa Kijijini kwao

C9 Wa Kiri Records, amedai kuwa yupo tayari na tayari ameshatoa mahari kijini kwao kwa ajili kuoa ingawa mwamke huyo alishawahi kuishi mjini miaka kadhaa.

C9 alidai kuwa alisafiri na kwenda nyumbani k

wa mama yake Songea vijijini na hatua ya kwanza aliyoifanya ni kumpa mama yake taarifa hiyo ya kutaka kuoa ingawa wengi hawakuamini baada ya kuwatamkia hivyo.

Hata hivyo alidai wapo ambao walidhani anatania kwani kasumba iliyopo huko ni kwamba vijana wengi wa mjini tabia zao si za kuoa kijijini kwani wanapenda sana wanawake waliyojipodoa na wale wanaovaa nguo fupi.

“Ni kweli nilisafiri kama unavyojua mzazi ukiwa hujamuona siku kibao lazima ukamtembelee na kuzungumza naye lakini kikubwa nilichokifanya kwanza ni kutangaza kuwa nataka kuvuta jiko awali walizani nafanya utani, na niliamua hivyo kwa sababu kuna mtoto nilikuwa nampenda kitambo sana hivyo huyo anaweza kuwa mke wangu endapo kila kitu kitaenda sawa,” alisema.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates