bonta |
Bonta a.k.a Maarifa hivi karibuni ameachia
wimbo wake unaoenda kwa jina la ‘Tukutane Maktaba’ ambao umesababisha maoni
mbali mbali kutoka kwa watu hasa kupitia mitandao ya kijamii kama facebook,
wengi wakimpa big up kwa kazi yake, lakini pia alipata criticism toka kwa Nikki
Mbishi wa Tamaduni Music ambae amekuwa akiandika status kuwamcriticise Bonta na
baadhi Weusi.
Mweusi toka katika kundi la River Camp
Soldiers alifanya interview na Josefly mtangazaji wa victoria fm iliyoko
Musoma, kupitia kipindi cha Over drive.
The river camp doctor alifunguka mengi
kuhusu ‘tukutane Maktaba’, kisha mtangazaji huyo aliuliza “baada ya kuachia
ngoma yako watu wengi walionekana kuipokea vizuri kupitia mitandao mbali mbali
ya kijamii na blogs mbalimbali, lakini kuna criticism, unamfahamu jamaa mmoja
anaitwa Nikki Mbishi?” Bonta alijibu “ah, hiyo no comment, hilo siwezi kuzungumzia kwa sababu kila mtu ana uhuru wa
kuongea kitu chochote anachotaka kwenye nchi yetu, kwa hiyo no comment kwa hilo
mtu wangu.”
Na kuhusu kile anachotamani kitokee kati ya
makundi yote ya hip hop Tanzania ambacho kingemfanya aone kakundi yamepiga hatua
Tanzania, alifunguka, “mi natamani kila kundi lifanye muziki wake na kila kundi
litumie miguu yake kutembea kufika pale linapotamani na lisitumie mgongo wa
kundi lingine, lisitumie midomo yao vibaya wala lisitumie freedom of speech
vibaya, kila mtu afanye kazi yake na kila aheshimu kazi ya mtu, au sio,
usitumie effort ya mtu ambayo ameshatengeneza ili upate negative publicity, at
the end of the day unajua mashabiki wako
ndio mashabiki wangu, mashabiki wangu wataendelea kuwa mashabiki wangu na
mashabiki wako wachache watakuja kwangu.”
Post a Comment