Baada ya tamasha kubwa la kiburudani Tanzania Fiesta
kumalizikia Dar kwa kumdondosha Rick Rossey ambae wengi hawakumdhania kama
angekuja, sasa ni muda wa kuanza
kuchambua kile ambacho kilitokea katika tamasha hili.
Idadi kubwa ya
waliopata nafasi ya kuona tamasha hili wameongea jinsi Rick Ross walivyofunika
na kuwakonga nyoyo watu wengi waliohudhuria katika viwanja vya leaders, Rossey
aliyepokelewa na mafataki wakati anapanda stejini, na kuendelea na shangwe za
mashabiki hadi mwisho wa show, inaonesha ni kweli aliweza kuuteka umati na
alipata feedback nzuri sana kuwa anakubalika sana Tanzania.
Lakini kama ilivyo kawaida zipo criticism toka kwa baadhi ya
watu waliohudhuria tamasha hilo ambao
pia naamini wanaweza kuwa ni moja kati ya watu walioshangilia na kuimba na Rick
Ross mwanzo mwisho lakini nao walikuwa na kitu moyoni mwao ambacho wameamua
kukisema baada ya show. Ni kweli kwa jina tu la Rick Ross lina maana kubwa sana
na inaweza kuwa ni sababu ya watu kushangilia sana, nyimbo wanazozipenda pia ni
sababu nyingine huku wakimuona mtu huyo huyo wanaempenda sana akiwa stejini.
Uwezo mkubwa wa kucheza na audience na kuwafanya wawe active mwanzo mwisho ni
baadhi ya uwezo aliouonesha Rossey, ila kuna kimoja ambacho wengi
wamekishangaa, ‘play back’ kwa msanii mkubwa kama huyu!
Wateja wa tamasha la fiesta waliohudhuria kwa wingi ili
kumuona Rick Ross kutoka Miami Marekani, wengi walishangazwa zaidi na kitendo
cha the Big Boss wa MMG kuimba kwa kundamizia nyimbo zake (play back) wakati
wanajua ni international artist, wakati kuna baadhi ya wanahip hop wa hapa hapa
Bongo kama Stamina waliweza kuimba juu ya beat chorus!
Wapo waliohoji inakuwaje wabongo wakienda huko nje ya nchi
wanaambiwa waimbe live wakati hawa wakija huku wenyewe wanakandamizia?
Ni kweli kabisa vita dhidi ya play back ni vita ambayo
wasanii wengi wa Hip Hop Tanzania wanaipagana ili wasound poa kwenye stage
badala ya kuuza tu sura stejini wakati CD inacheza wimbo mzima kama redioni.
Lakini moja kati ya sababu zinazopelekea wasanii wengi hapa
bongo kuimba juu ya nyimbo zao katika matamsha according to baadhi yao ni
kutoviamini vifaa vinavyotumika katika matamasha mbalimbali hasa yanayoandaliwa
na ma-promoter mikoani ambapo msanii anaenda bila kuwa na uhakika wa quality ya
sound na microphone.
Wapo ambao wengi tumewashuhudia hata mikoani wanafanya live
juu ya beat, ama kwa kutumia beat chorus, ama beat chorus yenye back vocal
kumpa support ama hata kuwa na mtu special wa kumfanyia back vocal.
Sasa turudi kwa Rick Ross, hii si mara ya kwanza kwa Rick
Ross kufanya play back, hata katika matamasha makubwa huko mtoni wenzake
wanaweza kuimba juu ya beat kavu lakini yeye mara nyingi hua anaimba juu ya
wimbo ila sauti yake kidogo inakuwa juu. Kwa hiyo sio kama alikuwa anadharau au
anaangalia ukubwa wa show kama ambavyo wengi wamecomment kuhusu hili.
Nimesema hili kwa sababu wengi wametoa maoni kama haya
kupitia facebook ambapo mmoja kati mashabiki waliohudhuria ameandika hivi
katika mjadala mrefu uliokuwa ukiendelea katika page ya Rama Dee kuhusu show ya
Rick Ross Fiesta 2012 :
“JAMAA[RICKROSS]MKALI
TU STUDIO KURECORD ILA KWENYE STAGE HANA RADHA,INAWEZEKANA NI DHARAU AU
KUMPAPATIKIA SANA KUKAMFANYA AFANYE KAWAIDA,CHA AJABU WANATAKA WAO WASANII WETU
WAKIENDA KWAO WAPIGE LIVE ILA WAO WAKIJA KWETU KITU CHA PLAYBACK SIKULITEGEA
KABSA,ZILE NI DHARAU COZ HUWA TUNAMUONA AKIWA KWAO HUWA ANAPIGA SHOW NZURI. ila
jana kashndwa hata kupumua mbele ya mtoto wa mji kasoro" STAAMINA"dah
mkali saaana.”
Ukiangalia BET Hop Hop awards ya mwaka 2011 aliingia kumpiga
tafu Meek Mill kuimba I’mm a Boss ambayo kashirikishwa lakini aliimba juu ya
verse zake za studio (play back), wakati katika tamasha hilo hilo DMX hakufanya
play back, T.I na Young Jeezy as well, Wizz Khalifa, DMX, Big Sean ambao wote
walitumia beat chorus hata Nick Minaj aliyeingia kumpa tafu Alicia Keys kwenye
show ya MTV VMAs ya mwaka huu aliimba live pia, wakati Jay-Z hua hana muda na
play back kama Rick Rossey.
Muonekano wa Rossey stage tu huwa unatosha
kuwapigisha watu shangwe za kutosha katika matamasha mbalimbali. Hata all I do
is Win ya DJ Khaleed Rick Ross hua anaimba juu ya verse zake wakati wanaperfom
wakati wenzake huwa wanapita juu ya beat wakisubiri chorus ya T-pain.
Post a Comment