CEO wa Bad Boy records P. Diddy ameamua kutumia vitendo
kuweka msisitizo katika taarifa kuhusu maendeleo ya afya yake siku tatu baada
ya kupata ajali ya gari maeneo ya Los Angeles.
Fans wa Sean Combs Diddy wa Dirty Money inaonekana wamepata
majibu kwa vitendo baada ya kali huyo kuamua kupiga misele kwa mguu katika
mitaa ya Hollywood huku akionekana yuko fit kiafya na anatembea kwa swag kama
kawaida yake.
Hii ni baada ya kuwashukuru fans wake na utawala wa juu wa
Los Angeles kwa sapoti yao kupitia account yake ya twitter siku moja kabla ya
kuonekana mitaani akipiga misele.
“The only reason I’m still here is through Gods Grace!!! Not
trying to be dramatic just being Real! God Bless All! Let’s go!,” alitweet
October 26, na akaongeza “ Thank you for all you prayers support and Calls!
Thank you for caring about a brother): I means a lot. Love yall!!! Let’s
go!!!”.
Taarifa iliyotolewa na watu wa karibu wa Sean Combs P. Diddy
baada ya ajali hiyo ya gari ilisema rapper huyo alipata injuries shingoni,
mbavuni na sehemu nyingine na alikuwa anapata matibabu nyumbani kwake akiwa
chini ya uangalizi wa daktari wake binafsi.
Inapendeza sana kumuona jamaa anapiga misele kwa miguu coz
fans wamepata majibu kwa vitendo kuwa yuko poa na mikandamizo itaendelea
kupitia Bad Boys Records.
God is Good, Combs ‘Let’s go!!!’
Post a Comment