Baada ya Rihanna kureveal cover ya studio
album yake ya saba yenye jina “Unapologetic” watu wengi walitoa maoni kupitia
mitandao ya kijamii kama facebook na twitter.
Album cover hiyo inayomuonesha Rihanna
akiwa hajavaa chochote juu (naked), picha hiyo inaambatana na maandishi mengi
kwenye mwili wake ambayo hayaeleweki japo mawili matatu yanaweza kusomeka
lakini bado hayatoi picha inayoeleweka haraka. Kiasi cha kufanya fans wahisi
labda ni majina ya nyimbo zitakazokuwa katika album yake, likiwemo jina ‘diamond’
na Unapologetic ambalo ndilo jina la album.
Katika picha ya album cover hiyo chuchu
moja ya Rihanna imefunikwa na maandishi wakati nyingine ikiwa ameifunikwa na
kiwiko chake cha mkono wa kushoto.
Watu wengi walitoa maoni mbalimbali baada
ya kupata details za album hiyo ambayo inategemewa kuachiwa rasmi November 19,
2012 na wengi walionesha kusifia sana cover yake hasa ile picha na baadhi ya
tweet za fans zilikuwa na maneno kama ‘I love that’, unapologetic sounds good‘
I’m so proud of her the cover and the name are totally Epic, Perfect, flawless
etc’, na mengine mengi ya kusifia.
Lakini kuna walioponda na kushangaa hiyo
cover iliyowekwa na wengine ikaonekana kama hii ni picha inayoonesha bad girl
Rihanna ambae ni unapologetic.
Post a Comment