Rapper the Game ambae alizinguana na kundi
la G-Unit na kuachana miaka mingi iliyopita amefunguka na kusema yeye ndiye
muuaji wa kundi hilo linaloongozwa na 50 Cent.
Rapper huyo ambae hivi karibuni alitangaza
kuwa amebatizwa na ameanza maisha mapya ya kiroho anaonekana kurudi nyuma
kidogo na kuwachokoza G-Unit kundi ambalo members wake wa zamani wote
waliondoka, Loyd Banks, Tony Yayo walifuata baada ya Game, lakini sasa 50 Cent
amewasaini wasanii wapya ambao kiukweli hawana moto kama wale members wa
zamani.
Game na 50 Cent waliingia katika mtafaruku
mkubwa sana katikati ya miaka ya 2000 na Game akaanzisha kampeni inayoitwa G-U
NOT. Na akasema kuwa 50 Cent aliandika wimbo wake ili aendelee kuwa juu kwenye
kundi kwa kuwa alikuwa na ‘umimi’ na akaeleza kwa nini alikuwa na hasira dhidi
ya 50 Cent na G-Unit. “300 Bars niliandika nikiwa na hasira sana na nilitaka
G-Unit ife brand kama brand, recording label, ama group…kuna msitari niliandika
ukisema you sell records but a G-G-G-Unot. Na baada ya hapo zikatoka T-Shirt na
harakati zikapiga hatua hata zaidi yangu.”
Lakini mwezi march mwaka huu Game
alipoulizwa kuhusu kilichotokea miaka hiyo kati yake na Boss wake 50 Cent,
alisema hiyo ilikuwa ni beef ya muda mfupi, “ilidumu
kwa muda wa mwaka mmoja au miwili hivi na ilinichukulia muda mwingi sana na
ilinifrustrate mimi na watu wengi. Kwa hiyo nilipoanza kuandaa album ya tatu,
ya pili na sasa nimeanza na hii ya nne nadhani busara kidogo ilitumika, na mimi
natokea Los Angeles na sikujiingiza moja kwa moja katika huo mtego” alisema
Game akimaanisha mtego wa hilo beef.
Akamaliza kusema anadhani hii inawahusisha
zaidi fans wao na wakosoaji wao na kile kilichoko kati ya maadui wawili ambao
walikuwa ni yeye na 50 Cent na kwamba sometimes asingeweza kucontrol hili.
Post a Comment