WEMA SEPETU BALAAA HII! ANGALIA PICHA NAMNA AKIMUOGESHA MREMBO KWA POMBE KALI


KATIKA kuonesha jeuri ya fedha, Wema Isaac Sepetu
amefanya kufuru kama kawaida yake baada ya kumlowanisha
mwili mzima kwa pombe za bei mbaya mrembo aitwaye Rehema Kimbu.

Mrembo Wema Sepetu
akimwogesha Rehema Kimbu kwa pombe.
Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa mwigizaji
Aunt Ezekiel, Mwananyamala, Dar, Ijumaa iliyopita
ambapo Wema na Aunt walimfanyia ‘sapraizi’ ya birthday 
Rehema ambaye ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.
Katika hali ya kushangaza, Rehema
ambaye ni shosti mkubwa wa Aunt
alishtukia anamwagiwa pombe mfululizo
aina ya Gordon’s na Jack Daniels huku
mwigizaji Nice Chande akimmiminia
chupa kubwa kadhaa za maji.

Muda mwingi Wema alikuwa akimmwagia Rehema
pombe bila kushusha mkono. Kufuatia kitendo hicho
kilichoambatana na kelele nyingi za mastaa hao,
kilisababisha wapita njia kujazana getini kwa Aunt
bila kujua kilichokuwa kikiendelea na kudhani
Rehema alikuwa akipokea kipigo.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates