Interview Na Producer Castro Baada Ya Miaka 10 Jela, Iko Hapa




Producer Castro [Castrol Ponella ] ametoka Jela miezi 5 iliyopita na leo nilipata nafasi ya kuzungumza nae kuhusu muziki na maisha yake kwa sasa. Ametoka 27 May 2013.

Ni producer aliyewahi kufanya kazi na rapper Queen Doren wa da Skendo, Mac 2 B, Fid q, Big Jahman, Spider na Akili The Brain.

Kwenye interview leo na eat radio Castro ameshukuru Wasanii na raia wote waliomtembelea alivyo kuwa jela na kusema kuwa ulikuwa wakati mgumu sana kwenye maisha  yake na sasa yeye ni mtu tofauti.

Castro ameniambia wakati anakwenda jela palikuwa na studio tano tu Dar es salaam, ameshanga sana kuona kila mtaa kuna studio na producers wamekuwa wengi sana.

Alikuwa akisikiliza Bongo Fleva sana akiwa jela na alipenda sana kusikiliza wimbo wa Darasa ft Winnie - Nishike Mkono Na ndio wimbo uliompa faraja sana akiwa jela.

Castro amesema anataka sana kuendelea kutengeneza Hiphop na msanii wa kwanza anataka kufanya nae Ni Darasa Na Fid q na ata taka wafanye Collabo. Fahamu kuwa Darasa amefurahi sana kusikia hivyo na ombi la Collabo na Fid q amelikubali sana na muda wowote yuko tayari
Kuhusu msanii anaye amini anafanya vizuri kwa sasa, Castro amesema Anamkubali sana Diamond na ni kwa sababu Diamond anajituma sana ndio  maana anamafanikio.

Zembwela, Big Jahman, Fid Q, Snali, Baucha na Akili The Brain ndio walimtembelea sana Jela ndani ya hii miaka kumi iliyopita.

Castro ameniambia kuwa kilichobadilika sana kwenye bongo fleva ni show nyingi zaidi,video za Bongo zimekuwa bora kwenye Production na muziki mzuri unaofanywa na vijana wa Hiphop.

Castro amesema hajakata tamaa ya maisha na anampango wa kuanza kazi ya muziki hivi karibuni na Jay Moe amempa Ushauri mzuri kuhusu maisha ya muziki na game kwa ujumla.

Castro anapatika facebook kupitia Castrol Ponella.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates