Ray C akimshukuru rais Kikwete Ikulu |
Rehema Chalamila a.k.a Ray C amemshukuru raisi wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa msaada wa matibabu yaliyomsaidia kwa
kiasi kikubwa kupona maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.
Mwana bongo fleva huyo aliyevuma na jina la ‘kiuno bila
mfupa’ pamoja na mama yake mzazi walifunguka wakati wakiwa katika maeneo ya Ikulu
ya Tanzania na wakiwa na raisi Jakaya Kikwete wakitoa shukurani zao za dhati
face to face.
Ray C aliyeooneka akiwa na afya inayoridhisha kwa kulinganisha na
hali mbaya ya kiafya aliyokuwa nayo katika siku za hivi karibuni, alimshika
mkono J.K na kumshukuru huku akisema yeye ndiye baba yake aliyemponyesha.
Mama yake Ray C naye pia alizungumza na kumshukuru Raisi
kikwete kwa msaada wake mkubwa na moyo wa upendo. Mama Ray C aliweka wazi kuwa
wale ambao walisema wanamchangia mwanae ili aweze kupata matibabu hajaona hata
shilingi yao bali aliyemsaidia ni Rais Kikwete.
‘Sogeasogea hitmaker’ ameahidi kuwa atarudi rasmi kwenye
game na kuwaburudisha mashabiki wake ambao kiukweli wamemmiss sana.
Hata hivyo Mwanamuziki huyo bado yuko chini ya uangalizi
maalum akiendelea na matibabu ikiwa ni muendelezo wa msaada alioupata toka kwa
Raisi.
Leotainmenttz.com Tunakuombea sana Ray C upone kabisa na
urudi kwenye game ili kuongeza safu ya wanamuziki wa kike ambao ni wachache
kwenye level za juu hapa bongo, tunamshukuru Rais wetu Kikwete kwa msaada wake.
Post a Comment