Miaka kadhaa imepita baada ya Kenya kukumbwa na balaa la
machafuko yaliyopelekea vifo vingi vya watu, majeraha ya kudumu na watu wengi
kukosa makazi yao baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 (post election violence).
Wasanii wa maigizo nchini humo wameshafanya filamu inayohusu matukio
yaliyotokea wakati huo na filamu inaitwa "Something Necessary".
Katika filamu hiyo wamemtumia character mmoja mwanamke
aitwae Anne ambae anaonesha maisha yake yalivyokuwa baada ya machafuko
yaliyoivuruga nchi hiyo mwaka 2007, Anne ni mwanamke anaehangaika kuyarudisha
maisha yake aliyokuwa nayo kabla ya machafuko hayo, akijaribu kupambana kwa
ajili ya afya ya mtoto wake wa kiume, alipompoteza mumewe, na shamba lake.
Lakini pia yumo character mwenye jina la Joseph, yeye ni
gang member aliyehusika katika machafuko hayo, lakini wote Joseph na Anne
wanajikuta wakiwa katika wakati mgumu wakitafuta jinsi ya kuzifuta kumbukumbu
hizo mbaya na kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Iangalie trailer yake hapa, "Something Necessary"...
Post a Comment