Mkali wa michano na ngoma zenye maisha marefu Roma Mkatoliki
toka Tanga ameonesha kuwa ameusikiliza kwa makini na kuuelewa wimbo mpya wa
Stamina 'Wazo la Leo' aliomshikirisha Fid Q, na kuchagua kuiandika tena kwenye
ukurasa wake wa facebook mistari inayopatikana kwenye verse ya pili ya ngoma
hiyo.
Roma ameandika status yenye mistari hii,
"bora uitwe
mfalme juha kwenye utawala wa kishamba
mapenzi yakikusumbua tafuta daktari wa KITANGA
#STAMINA# tisha shoro bwenzi!!!
Mistari hii ipo kwenye verse ya pili na ni mstari wa tatu na
wa nne. Jinsi Stamina alivyoitaja Tanga itakuwa imemgusa Roma ambae sasa hivi
yuko mitaa yake ya home Tanga, japo naamini ameguswa na mistari mingine pia au
hata wimbo mzima.
Roma ni msanii ni kati ya wasanii ambao mara kwa mara
wamekuwa akitumia wall zao kuwasapoti baadhi ya wananii wa bongo anaowakubali,
mwaka jana ilipodondondoka Dear God ya Kala Jeremiah alimpa shavu kwenye
ukurasa wake wa facebook kuwa watu wakamwambie kuwa amemuelewa.
Anyways, ilikuwa ni maandishi ya appreciation kupitia public
coz watu wangesema kama vipi angempigia hata simu amwambie mwenyewe,ila hii
ilikuwa inaambatana na sapoti yake kwa Kala kupitia fans wake pia.
Hivi karibuni Roma aliachia wimbo wake mpya "2013"
na uliongoza kwa kuwa downloaded kwenye mitandao mbalimbali na unaendelea
kufanya vizuri.
Post a Comment