Justin Bieber hajapenda mama yake kufanya project ya filamu ya kupinga utoaji mimba.


Siku chache baada ya mama mzazi wa mkali wa pop na R&B Justin Bieber kutangaza kuwa anatengeneza filamu fupi ya kupinga utoaji mimba (anti-arbotion), inasemekana kuwa Justin Bieber hajapenda project hiyo mpya ya mama yake.


Kwa mujibu wa Chicago Sun Times, mwimbaji huyo mwenye umri mdogo hajapenda project hiyo kwa sababu imebeba mambo ya kisiasa.
Mtu wa karibu wa Biebs aliliambia Chicago Sun Times kuwa Justin hapendi mambo ya kisiasa kama utoaji mimba ambao kwa upande wa Marekani ni issue nzito sana iliyojaa siasa. Chanzo hicho kilisema kuwa Biebs ameegemea zaidi katika kuwaburudisha fans wake na havutiwi kabisa na agenda za kisiasa. Amesema amechoshwa na kukutana na vichwa vya habari ambavyo ni vinahabari mbaya zinazomhusu yeye.

Mama yake Bieber Pattie Mallette alitangaza hivi karibuni kuja na project mpya ya filamu inayoitwa "Crescendo" inayopinga utoaji mimba, akiwa na lengo la kuwahamasisha vijana kufahamu kwamba kuna sehemu ya kwenda ambapo watu watawatunza na sehemu ya kuishi kama watapata ujauzito na wakaona hawana sehemu ya kuegemea.


Crescendo inatarajiwa kuoneshwa kwa mara ya kwanza february 28,na waandaaji wa filamu hiyo wamepanga kukusanya pesa kiasi cha $10 million kwa ajili ya vituo vya kuwahudumia wajawazito.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates