Msanii wa muziki Bon Eye kutoka kundi maarufu la P Unit, ameweka wazi
kuwa mbali ya kuwa rapa mkali, yeye pia ni mwigizaji mzuri sana na pia
DJ ambaye pia alikwishapiga muziki katika kumbi mbalimbali za starehe
kabla ya kutusua katika muziki.
Msanii huyu amesema kuwa katika historia yake ya uigizaji, alikwishawahi pia kuwa mwandishi wa michezo ya maigizo na alikuwa mstari wa mbele katika uigizaji kipindi alipokuwa shule ya sekondari ya Kajiado huko Kenya.
Kutokana na vipaji hivi vikubwa rapa na mwigizaji huyu ameweza kujiweka katika nafasi nzuri kwenye ramani ya burudani Afrika Mashariki akiwa ni moja ya kichwa kikali chenye mchango mkubwa ndani ya kundi la P Unit
Post a Comment