Baada ya kumaliza ziara yake ya muziki Marekani, Msanii wa muziki kutoka
lebo ya Grandpa Jijini Nairobi, DNA kwa sasa anajipanga kwa ajili ya
ziara nyingine kubwa nje ya nchi, ambapo safari hii ataelekea huko Dubai
pamoja na UK kwa ajili ya maonyesho kadhaa.
Ziara hii ya DNA inatarajiwa kuanza mapema mwezi ujao na hii ni baada ya kupata mualiko kwenda kutumbuiza umati wa mashabiki ambao wengi wao ni raia wa Kenya wanaoshi huko Ughaibuni.
Taarifa hii inakuja sambamba na habari njema kwa Lebo ya muziki ya Grandpa ambayo pia mwishoni wa wiki imefanikiwa kushinda tuzo ya lebo bora ya muziki Afrika Mashariki kutoka Wynton Music College, tuzo ambayo imezidi kuwaongezea motisha kuongeza nguvu kusaidia wasanii wenye vipaji Afrika Mashariki.
Post a Comment