Lebo ya muziki inayokuwa kwa kasi sana Afrika Mashariki, Grandpa kutoka
Kenya, imefanya hatua nyingine ya nguvu kwa kumsaini nyota mwingine
mkali wa muziki wa nchi hiyo, Kenrazy ambaye sasa anaungana na timu hiyo
ambayo siku hadi siku inajizolea heshima kwa kazi nzuri inazofanya.
Huu ni ujio mpya na wa faraja wa Kenrazy ambaye wengi walikuwa
wakifahamu kuwa amekwishastaafu muziki, ambapo hatua ya msanii huyu
kuingia Grandpa imeenda sambamba na kuachia kazi mpya inayokwenda kwa
jina 'Vitambi'.
Kenrazy bado anajulikana kwa ngoma yake kali ambayo inakwenda kwa jina
Ti-Chi, na sasa akiwa chini ya Grandpa, Msanii huyu anatarajiwa
kurudisha heshima aliyokuwa nayo katika muziki katika ngazi aliyokuwa
amefika hapo awali na zaidi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment