Latest Updates
NEWS- WATANZANIA WANAOISHI NCHINI UK WAMEFANYA HIKI ILI KUSAIDIA WATU WENYE UALBINO
PICHA - WANAUME WA JAPANI WAMESOMA KOZI HII ILI KUVUTIA WANAWAKE
Najua kuna watu wangu ambao sasa wapo kwenye mchakato wa kuoa au ndio wanatafuta mtu ambaye wataishi nao, lakini inawezekana kumekuwa na changamoto, Sasa leo September 20 2016 nakusogezea hii inayotokea nchini Japan ambapo wanaume ambao bado hawajaoa wanahudhuria kozi ya kulea watoto ili kumvutia mwanamke zaidi.
Bachelor hao wa kijapan wamehudhuria kozi ya kulea watoto ili kuongeza nafasi ya wao kupata wapenzi, Mwalimu wa kozi hiyo Takeshi Akiyama amesema lengo la kozi hiyo ambayo imeandaliwa na Ikumen University ni ili kusaidia mtu ambaye hajaoa kupata mke.
Masaya Kurita (31) bachelor anayeishi Tokyo Japan ameanza kozi baada ya kutafuta mke kwa miezi sita iliyopita, Aidha anaamini kuwa kufanya mazoezi ya kulea mtoto kwa kutumia plastiki kunaboresha nafasi yake ya yeye kukukbalika kwa mpenzi .
NEWS - MTEMVU ASHINDWA KESI YA UBUNGE TEMEKE
Aliyekuwa Mbunge wa Temeke (CCM) Abbas Mtemvu, ameshindwa kesi ya uchaguzi dhidi ya Abdallah Mtolea(CUF) aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana.
Mtemvu aliyekuwa akitetea kiti hicho katika uchaguzi Mkuu wa mwaka jana alifungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akipinga matokeo yaliyompa ushindi Mtolea.
Pamoja na mambo mengine akidai kuwa kura za baadhi ya vituo vya kupigia kura hazikujumlishwa katika matokeo ya jumla.
Hata hivyo Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Issa Maige aliyekuwa akisiliza kesi hiyo imetupilia mbali madai ya Mtemvu na badala yake imemthibitisha Mtolea kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.
Katika hukumu hiyo Jaji Maige amesema kuwa Mtemvu ameshindwa kuthibitisha madai yake jinsi yalivyoathiri ushindi wa mbunge huyo, huku akisema kwamba kasoro alizokuwa akizilalamikia Mtemvu hakuathiri ushindi wa mbunge huyo.
News wasiokua na uraia wajadiliwe
Tanzania imeitaka jumuiya ya kimataifa kujadili tatizo la uwepo wa watu ambao si raia wa nchi yoyote ile.
Pendekezo hilo limetolewa siku ya Jumanne na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga ( Mb) katika mkutano wa Kilele wa viongozi kuhusu wakimbizi.
Mkutano huo uliandaliwa na Rais wa Marekani Barack Obama kwa ubia na nchi za Ethiopia, Jordan, Mexico, Sweden, Canada na Ujerumani ambapo nchi 60 zilialikwa,45 kati ya zilizoalikwa ikiwamo Tanzania zilitoa ahadi ya namna moja ama nyingine.
Nchi hizo ni zile ambazo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa zikiwapokea na kuwahifadhi wakimbizi, zimekuwa nchi za mpito kwa wakimbizi, au zimekuwa zikitoa misaada ikiwamo ya hali na mali pamoja na kuwapatia uraia, ajira na misaada ya kibinadamu.
Lengo kuu la mkutano huo wa viongozi kuhusu wakimbizi lilikuwa ni kwa nchi kutoa ahadi mpya ambazo kwayo zitasaidia katika kuwapatia fursa za ziada wakimbizi ili pamoja na mambo mengine kuwapunguzia changamoto zinazowakabili na kuwafanya wajisikie na kujiona kuwa nao ni binadamua kama binadamu wengine.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Waziri Mahiga, amesema, Tanzania kutokana na jiografia ya nchi hiyo ilivyo imejikuta mara kwa mara ikiwa ni kimbilio la wakimbizi kutoka nchi jirani.
Akawaeleza washiriki wa mkutano huo, kwamba, suala la Tanzania kuwahifadhi wakimbizi ni la kihistoria na halikuanza jana au juzi.
“ Tanzania kutokana na jiografia yake imejikuta ikiwa ni kimbilio wa watu wanaotafuta salama ya maisha yao. Tumekuwa tukiwapokea na kuwahifadhi wakimbizi tangu miaka ya 60. Na tunatekeleza jukumu hilo kwa kuzingatia sheria za kimataifa na mikataba ya kimataifa, na sheria zetu za ndani” akasema Mahiga.
Na kuongeza kwamba, Tanzania itaendelea na jukumu hilo pale itakapopashwa kufanya hivyo kwa kufuata na kuzingatia sheria za nchi na sheria za kimataifa.
NEWS - VIPENGELE TUNZO ZA EATV AWARDS VIKO HAPA
Vipengele vya tuzo mpya zilizoanzishwa na kituo cha runinga cha East Africa Televisheni, EATV Awards, vimetangazwa Ijumaa hii.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Mkuu wa masoko wa kituo EATV,Roy Mbowe alisema tuzo hizo zitakuwa na vipengele 10 zitakazohusisha muziki, filamu na tuzo moja ya heshima.
Vipengele hivyo ni:
1. Mwanamuziki bora wa kiume
2. Mwanamuziki bora wa kike
3. Mwanamuziki bora chipukizi
4. Kundi bora la muziki
5. Video bora ya muziki
6. Wimbo bora wa mwaka
7. Muigizaji bora wa kiume
8. Muigizaji bora wa kike
9. Filamu bora ya mwaka
10. Tuzo ya heshima itakayotolewa kwa mtu au kampuni iliyochangia kwa kiasi kikubwa katika kazi za muziki.
Mbowe amesema kazi za sanaa zitakazoruhusiwa kuingia kwenye vipengele ni zile zilizotoka kuanzia Julai 1 2015 – 30 Juni 2016. Tofauti na tuzo zingine, wasanii wanaotaka kushiriki watalazimika kujaza fomu za kutaka kutajwa kwenye tuzo na kuwasilisha kazi husika ambapo mchakato wa uchambuzi wa kazi hizo utachukua kipindi cha mwezi mmoja kabla ya majina yaliyoingia kwenye tuzo hizo kutajwa na kuanza kupigiwa kura.
Hata hivyo amedai kuwa pamoja na wananchi kupiga kura, kutakuwepo na jopo la majaji litakaloshiriki kupata washindi. Tuzo hizo zinazodhaminiwa na kampuni ya Vodacom, zitatolewa December 10 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
News- bila wivu hakuna mapenzi jux
Msanii Jux ambaye sasa ni mpenzi wa Vanessa Mdee amefunguka na kusema kuwa wimbo wake mpya 'Wivu' ambao unafanya vizuri kwa sasa hajaimba kwa ajili ya mpenzi wake Vanessa Mdee.
bali ameimba wimbo huo kutokana na hisia kwani jambo hilo linawakuta wengi ambao wanapendana kweli katika mahusiano yao ya kila siku.
Jux akizungumza kwenye kipindi cha ENEWZ ya EATV alidai kwenye mapenzi kama hakuna wivu kati ya wawili wapendanao hapo kunakuwa hakuna mapenzi ya kweli kati yao kwani wivu ndiyo ishara ya upendo wa kweli.
"Wimbo wa Wivu ni matukio ya kimapenzi ambayo yanatokea kwa watu wengi ila siyo kama nimejiimbia mimi, unajua kabla sijarekodi wimbo ule tukiwa studio niliwauliza wakina Bob Manecky na wengine jamanii mnadhani 'idea' hii inaweza kuwa sawa ndipo hapo wakaniambia ni wazo zuri kwani kwenye mapenzi bila uwepo wa wivu kuna kuwa hakuna mapenzi ya kweli, ndiyo hapo nikajua kumbe suala hili linawagusa watu wengi" alisema Jux.
Mbali na hilo Jux amesema kuwa hivi sasa muzuki unakuwa kama haupo kutokana na ukweli kwamba watu wanatanguliza life style mbele kuliko hata kazi zao na ndiyo maana wasanii wengi wakitaka kutoa kazi zao wanafanya mambo mbalimbali kutafuta kiki ili waweze kutambulisha kazi zao hizo.
"Sipendi sana kuulizwa maswali juu ya Vanessa napenda niulizwe maswali juu ya kazi zangu mimi kama msanii, ili nitangaze kazi zangu mimi ndiyo maana kuna vitu saizi sisi tunavikwepa kwa makusudi, tunataka kurudisha muziki hivyo mambo ya kiki, life style tunataka yakae pembeni" alisema Jux
NEWS- watakao sambaza Ky kukiona
MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali (NGOs) ambayo yatabainika yanaendelea kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, yatafutiwa usajili.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aliyaandika hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa ‘facebook’.
Alisisitiza kuwa serikali italisimamia suala hilo kwa ukamilifu.
“Sijapiga marufuku matumizi ya vilainishi, ukweli nimepiga marufuku mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kununua na kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi na wanaume wenzao na sababu nimeshazieleza,” aliandika na kuongeza:
“Na nafurahi kuwajulisha kuwa tayari baadhi ya mashirika hayo yameanza kutekeleza agizo hili kwa kuondoa vilainishi kwenye miradi yao. Nayapongeza sana. Niendelee kuyataka mashirika mengine kutii agizo hili ambalo tutalisimamia kwa ukamilifu.
“Serikali haitasita kuchukua hatua ikiwamo kuyafutia usajili mashirika yanayoendelea na miradi ya kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja”.
Aliyataka mashirika hayo kushirikiana na serikali kupambana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kujikita kwenye afya nyingine inayozingatia sheria za nchi na mila na desturi za Watanzania.
Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni, Waziri Ummy alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kubaini matumizi ya vilainishi hivyo yanachochea kuongezeka vitendo vya ushoga ambavyo ni kinyume na sheria za nchi.
“Lengo pia ni kudhibiti maambukizi ya VVU kwa sababu katika wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, asilimia 23 tayari wana maambukizi hayo.
“Tumebaini baadhi ya wadau wanaotekelezeka shughuli za makundi maalum wamekuwa wakikiuka taratibu za utendaji na kusambaza vilainishi hivyo.
Awali agizo hilo lilizua mjadala mkubwa katika mitandao ya jamii, wengi wakikosoa uamuzi huo wa Serikali kupiga marufuku vilainishi hivyo.
Walisema kwamba vinatumika katika mambo mengine mtambuka hususan hospitalini huku wengine wakisema viendo vya ushoga havichangiwi na kuwapo vilanishi bali ni mmomonyoko wa maadili uliotamalaki nchini
News- ngumbe & Salu T kuja na ngoma ya pamoja
Baada ya kila mmoja kufanya poa kwenye ngoma zake artist toka lebo ya mandev records wameamua kuja na muunganiko usio rasmin baada ya kuamua kufanya ngoma ya pamoja.
Wakiongea na chiwileinc Ngumbe amesema lengo ni kuchanganya mziki wa hip hop wenye ladha tofauti
"Unajua Salu t anafanya hardcore Mimi nafanya comecial tumeona iv vitu tukiviweka pamoja vitaleta kitu tufauti kwa mashabiki wetu"
NEWS - Sirudi tena nyuma: Nuhu Mziwanda
NEWS - Mesen Selecta asakwa na Polisi
Panya anayegundua mabomu
Panya anayegundua mabomu Afrika
'Panya mwokozi wa maisha'
Shirika moja lisilo la kiserikali la Ubelgiji APOPO limeanza
kuwafundisha panya namna ya kutambua mabomu yaliyofukiwa ardhini. Panya
hao ambao ni wakubwa kuliko panya wa kawaida wanafanyiwa
majaribio Morogoro Tanzania .Inaaminika wanauwezo mkubwa wa kunusa
kuliko mbwa. Hii inatokana na kuwa pua zao zipo karibu na ardhi,hali
ambayo inawasaidia katika kazi yao ya utambuzi wa mabomu
Grandpa yamnasa Kenrazy
BAADA YA JOBFIRE KURUDI KWAO MOSHI NA KUSEMA MZIKI MGUMU TOWN SOMA ALICHO AMBIWA NA HAMMER Q
hammerq Fire
?? Katika maisha hakuna kitu kibaya km kukata tamaa, na ukumbuka xana
maneno yangu kwamba Askari hatakiwi kurudi nyuma wakati wa vita
anatakiwa asonge mbele kupambana na maadui sababu bila ya kupambana hawezi
patikana mtu anaeitwa SHUJAA huwezi itwa shujaa kama hujapambana ,FIRE
unatakiwa kurudi twn kuja kukamilisha melengo yako, mziki sio lelemama
mwanangu unahitajika ukaze roho na misuli yote mwilini tuliza akili yako
fire mziki unaujuwa na unauweza ila jifunze xana kupigana na moyo
wakukata tamaa kumbuka mafanikio hayaji kwa siku mojaJobfire Mkali nimekuelewa baba yangu ila usijali kuna mazingira nayatengeneza ili nipate kujiweka ktk nafasi fulan baba yangu najua unataman sana kuona mwanao nikifika mbali kimuziki ila ucjal baba yangu
Keko amzingua Linex?
Mwasiti, Shetta watoa usia
Mansu Li kutambulisha kichupa





.jpg)



