ZUNGUKA kumbi zote za disko. Hautamuona mwanasoka yoyote wa Tanzania amemshika kiuno mwanamke maarufu (celebrity) katika fani yoyote maarufu kuanzia, filamu, muziki hadi siasa. Na sio hao tu, wanasoka wa Tanzania wanaishi dunia tofauti na wanawake wenye hadhi za juu (high Personalities female)
Wakati David Beckham akihangaika na Victoria Adams, Cristiano Ronaldo akihangaika na mwanamitindo wa Kirusi, Irina Shayk, hali ni tofauti kwa mwanasoka wa Tanzania. Ni nadra kwenda katika klabu ya usiku (Nightclub) na kumkuta Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akiwa katika mtoko na Mwanamitindo Flavian Matata. Unajua kwa nini kuna sababu nne kubwa. Kwanza ni umaskini unaowakabili. Hawapo katika kiwango cha kushindana kifedha na mastaa wa fani nyingine ndani ya nchi. Wakati mwanamuziki Diamond anaweza kuingiza sh 30 milioni kwa shoo za mwezi mmoja, inamchukua Mrisho Ngassa miaka miwili ya kusaini mkataba mpya ndipo apate fedha hizo.
Wema Sepetu hawezi kwenda kwa Mrisho Ngassa. Atakim
bilia kwa Diamond kwa sababu anajua wanaweza kuagiza chochote wanachojisikia katika hoteli yoyote ya hadhi ya nyota tano bila ya hofu.
bilia kwa Diamond kwa sababu anajua wanaweza kuagiza chochote wanachojisikia katika hoteli yoyote ya hadhi ya nyota tano bila ya hofu.
Mwanadamu anayesubiri shilingi 30 milioni baada ya misimu miwili ana tofauti kubwa na mwanadamu anayesubiri shilingi 30 milioni baada ya wiki tatu. Kwa Ulaya na kwingineko, hali ni tofauti. Wanasoka wameingia katika soko la ushindani wa kimaisha na wasanii na mastaa wengine kutokana na mapato makubwa wanayotapata ndani ya fani zao, na katika matangazo ya biashara.
David Beckham, Kanye West na Tom Cruise wote wanaweza kununua nyumba katika mtaa mmoja wa Beverly Hills, ni wazi kwamba wote wapo katika nafasi sawa ya kutoka kimapenzi na Kim Kardashian bila ya kujali kama Kanye West amemuwahi.
Lakini pia sababu ya pili ya msingi inayowanyima fursa wanasoka wetu ni makuzi waliyopitia ambayo yamewanyima fursa katika elimu na tabia ya kujiamini katika maisha yao. Wengi wao wamekosa uwezo wa kujiamini, kujitawala kifikra na kujiamulia mambo kwa uhuru. Utaongea nini mezani na mrembo anayejiamini huku akinywa Savannah yake taratibu.
Wakati pesa likiwa tatizo la kimsingi, bado upeo wa fikra kichwani ni tatizo jingine linalokusumbua ukikaa na mrembo aliyemaliza chuo kikuu au IFM miaka sita iliyopita. Unahitaji kuwa zaidi ya Jerry Tegete. Zaidi ya mabao, una nini mezani. Pesa au elimu?

Zaidi ya yote haya. Wanasoka wa Tanzania wametoka Ghetto. Ni wachache waliotokea katika familia zinazoeleweka kwa sababu mchezo wa soka bado unabakia na taswira kuwa ni mchezo wa kihuni na ni watu wa hali ya chini.
Zao linatoka katika picha hii iliyopo kuhusu soka, lazima litamtoa mwanasoka ambaye kichwa chake kwa asilimia nyingi kinafikiria uhuni na kushindwa kujiamini katika fursa zilizopo. Mwanasoka aliyetoka katika familia isiyoeleweka hawezi kujipa hadhi sawa na ya kujiamini mbele ya Mwanamitindo anayefanya kazi zake London, Paris, Milan na kwingineko na ambaye amelelewa katika familia njema.

Mpaka wanasoka wa Tanzania watakapoanza kutoka nje ya mipaka yao na kuelimika nadhani watajipa nafasi nzuri ya kuanza kutoka kimapenzi na celebrities wa kike. Ni kwa sababu wakiwa nje watakuwa kama wako darasani huku wakielimika na kujiongezea uwezo mkubwa wa kujiamini.
Nje, wanasoka wanafundishwa jinsi ya kujiamini, jinsi ya kuongea, jinsi ya kujitawala na jinsi ya kujipenda. Na zaidi ya yote watalalia paundi nyingi na Dola ambazo zitajikuta zikiongea zaidi kuliko midomo yao!
Post a Comment