Madee amesema pamoja na show za kawaida, makampuni ya simu yameshamsainisha show zaidi ya 12 ambazo zimekuwa zikimpa mkwanja wa nguvu.
Akiongea na mwandishi wetu, Madee amesema pia muziki wake umetoa fursa kwa vijana wa Tip Top Connection ambao amekuwa akifanya nao kazi katika show mbalimbali.
“Nimekua nikiingiza Milioni 2 hadi 3 kwa wiki kutokana na Pombe Yangu. Ni tofauti na awali wakati tunaanza muziki kwa sasa ukifanya wimbo ukawa mkali basi ujue pesa zipo zinakusubiri. Pamoja na hayo wimbo ya Pombe Yangu umetoa fursa kwa vijana ambao nakuwanao kwenye show zang. Filamu ya “Pombe Yangu” pia imeajiri vijana,watu wametengeneza T-Shirt ‘Nani kamwaga Pombe Yangu’. Hiyo ni fursa wameitumia kupitia Pombe Yangu, alisema Madee.
Post a Comment