ALL IN ALL SEHEM YA 2

HII NI SIMULIZI HAIHUSIANI NA MTU YOYOTE YULE NI TUNGO TU NA KAMA IKITOKEA BASI NI MIPANGO TU YA SIR GOD.
mara simu ya Yahya iliita   "Oyo sasa me nasepa namuwahi huyu mana do ananiharakiza kama vipi nitgakutafuta mana nimesikia tangazo redio kuwa wanatafuta vipaji vipi umesikiaa" Rashid alionekana kuduwaa  "hapana sijasikiaa....."  Rashid alijibu kwa haraka "basi sawa nikirudi nitakuambia... " Yahya alijibu huku akiwa katika harakati za kuondika maeneo yale "kaka fanya kuniambia japo kidogo basi mana tayari ushaniitia hamu.."  Yahya hakutaka kumdokeza hata kidogo kwa kuwa alikua na haraka ya kufata yule mwana mke wake, baada ya Yahya kupinda katika Rashidi alirudi katika foleni ya maji huku akiwa na mawazo iliyoambatana na njaa isiyo ya kawaida iliyochanganyika na machofu mara nyingi alikua akipiga ming'ayo. "naomba jamani hii ndo moja tu mana mtoto analia nyumbani..." Sauti ya mwanamke ambae

anaonekana amekula chumvi kidogo iliskika, Rashidi hakuwa mchoyo watu wengi sana walivutiwa na tabia
yake ya uchangamfu na umaridadi wake licha ya kuwa kwao masikini lakini alipenda kuwa maridadi, lakini hapa alikuwa akikereka ndani ya nafsi yake bila kuonesha hata usoni kwa kitendo cha yule Mzee kutaka kusaidiwa kuchota maji kwa mda ule mana yeye alishapoteza mda mkubwa sana kusubiri zamu yake ifike.  "akhaa! jamani si amesema anataka ndoo moja tu sasa inakuaje na nyengine tena ??" Rashid alijikita akiongea kwa sauti wakati huu baada ya ndo ya kwanza ya yule bibi kujaa na sasa alikuwa anaweka ndoo nyengine. "mjukuu wangu naomba kumaliza na hii moja tu..." Rashidi hakumjibu kitu wala wale watu wengine hawakusema chochote, alikosha ndoo yake yule Bibi na kuiweka katika mfrereji. Baada ya mda kidogo kupita zamu yake Rashidi alifika yeye alikua na madumu ya lita 20 manne aliyachotea maji na kuondoka zake uzuri ni kwamba mfereji haukua mbali sana na nyumba aliyokuwa akiishi. "mbona umechelewa sana au ulipita safari zako?' Bi key alimuliza Rashidi "hapana kulikua na watu wengi sana iyo ndo sababu iliyonifanya nichelewe" Rashid alijibu huku akishusha pumzi. "pole mwanangu ndo maisha chakula kipo tayari" Bi key aliingiwa na huruma kwa mwanawe kwani alijua wazi wazi kuwa mwanawe alikua amechka sana, Rashidi aliingia ndani na kuweka yale madumu kendo cha pili alitafua chakula na kutoka njee kwani giza limeshaingia pia kulikua na kibatari kimoja tu kwani nyumba yao haikuwa na umeme, sasa alikua amekaa na mama yake pale barazani mbele ya nyumba yao hapa kitu cha ugali na mchuzi wa dagaa kauzu kilihusika, "si ungeenda kukoga na ubadilishe izo nguo ndo ule?" Bi key alimuliza Rashid "mama hapa kama utaniamiamini tangu asubuhi sijatia kitu chochote kinywani nini njaa balaa hapa"  Bi key alikosa la kusema ila alikua akimuangalia mwanae usoni mara kwa mara bila ya Rashidi kujijua na kumuhisi kama anaufahidia ule ugali, Bi key mara nyingi alipenda kusikiliza redio ila hakupenda sana kusikiliza mziki wa kizazi kipya ingawa baadhi ya nyimbo alizipenda sana kwa mdaa huu wa saa tatu hakujua asikilize chanal gani tangu kimalize kipindi cha Raha utamu kutoka Coconut FM na Ali Nahoda alikua akibadilisha chanal mara kwa mara. "mama ndo umeweka redio gani hebu nipe mimi" Rashidi alimuliza mama yake ila Bi key hakumjibu chochote na kumpa ile redio ndo ambayo inatumia bettry. Moja kwa moja aliweka masafa ya 90.9 Chuchu FM na kukumbana na kipindi cha East African Flever kwa sasa ilikua ni majira ya saa 9 na nadika 17 wakati huu alikua akiongea Chiwile presenter kutoka katika hiyo redio...........

USIKOSE KUFATILIA SIMULIZI HII SEHEMU YA 3 JUMANNE IJAYO     

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates