Home
»Unlabelled
» SOMA STUTAS YENYE HISIA KALI KUTOKA KWA ROMA
SOMA STUTAS YENYE HISIA KALI KUTOKA KWA ROMA
By
Unknown
•
9:39 AM
•
•
Ilikuwa
siku ya tarehe 12th september 2002, siku ya alhamisi kama leo,
majira ya saa 4 hivi asubuhi!!!(mida kama hii ninayoandika status hii)!!
Tukiwa hospital TANGA (Bombo hospital)!! kitandani akiwa amelala
BABA YANGU MZAZI, na pembeni tukiwa tumemzunguka WATOTO WAKE/MAMA
YETU/BIBI YETU(ambaye ndiye mama yake baba)!!...
tena
nakumbuka bibi alikuwa akikusanya vitu pale wodini,chupa ya chai na
vyombo na baadhi ya nguo, as if tunaondoka kurudi nyumbani(bila shaka
alishakata tamaa na mgonjwa wake)!! maana hata alipoulizwa kwanini
vile!!? alijibu kwa lugha ya kikwao "kipare" kuwa leo tunarudi
nyumbani na dalili ya unafuu hajaiona!!!
"watu wazee wanaona mbali sana"!!
Kiukweli kila mtu hakuwa na raha wala amani asubuhi ile...ni kama tulikosa raha wanafamilia wote pale!!
wakiwa wanamlazimisha baba anywe uji kidogo hata asubuhi ile aongeze nguvu!!!
Mungu huyu ni wa kumtukuza siku zote!!
nakumbuka nilikuwa kidato cha pili mwaka huo, lakini sikumbuki hata kwanini sikwenda shule, sina kumbukumbu hiyo!!
Ghafla nikiwa kwenye kochi nimekaa pembeni nachezea chezea simu, nikasikia mama akipiga kelele huku akilia.......
"usiniache usiniache usiniache"......
nashtuka na kuangalia kitandani....OOOH GOD!!! nilichokiona ni
picha ambayo hadi leo miaka 11 imepita, lakini picha hiyo inajirudiaga
katika akili yangu kila mara!!
ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kushuhudia mtu akiwa anaaga dunia!!!
"SIKU ZAKE ZILIFIKA"
na hali ya pale wodini haikuwa tena ya kawaida, ni vilio na kutokusikilizana...
ILA UKWELI NI KUWA BABA ALIKUWA AMESHAFARIKI ASUBUHI HII!!
WISH KAMA UNANISIKIA DADDY!!
- We all cool sasa/ tupo wazima watoto wako wote, na mama anatutunza vema!!
-Dadii nimekuwa sasa mwanao, A GT BABY BOI na anaitwa IVAN (Gift from
god)!! ikiwa na maana kuwa ujio wa mtoto huyu wa kiume ktk familia ni
sawa na mimi kumuona BABA, na sawa na MAMA kumuona mumewe na ndio maana
mama humuita ivan MUME WANGU!!
-Hey dadii nimekuwa msanii
mkubwa kiasi sasa tofauti na kipindi unaniacha, ukiwa unanizaba makofi
nikifuta kanda zako za Madilu system/Aurlus mabele/Bozi boziana/Awilo
longomba kisha najirecord nikichana akapela!!!
ile imenijenga na sasa NAIFUNGA SHOW MIMI LEO!! na inanipa maisha kazi hii!!
-BABA kuna mengi tu ya kuongea ni hivo hatujapewa uwezo huo na aliyetuumba!! ila tunakukumbuka sana wanao-:
Rasheed/Omar/Maimuna/Asha/ R.O.M.A!!!
leo umetimiza miaka 11 kaburini!!! kila siku tunakuombea na tutazidi kukuombea milele yote!!....
R.I.P DADY....a wish ungekwepo/tucelebrate anakumiss mke wako!!!
"KUNA KABURI LA BABA NITARUDI KILIMANJARO"
Rooomaaa!!!
SIMILAR ARTICLES
Post a Comment