MTANGAZAJI wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani wa Redio yaTimes, Khadija
Shaibu ‘Dida’ hivi karibuni amefungukia madai ya kwamba ana mimba ya
mumewe wa sasa, Edzen Jumanne na kwamba mfumo wake wa kimaisha hasa
kwenye ulaji umebadilika.
Khadija
Shaibu ‘Dida’ Katika picha kapakatwa.
Juzikati, chanzo
ambacho ni rafiki wa Dida kilichoomba hifadhi ya jina lake kilisema:
“Unajua mwanamke mwenye mimba hajifichi, Dida atakuwa kishapachikwa,
nyie fuatilieni.”
Katika kujua ukweli wa jambo hili la kheri,
mwandishi wetu alimtafuta Dida na katika maelezo yake alidai kuwa
taarifa hizo hazina ukweli kwani bado hawajapanga suala la kuzaa
kutokana na mumewe kuwa na mtoto mdogo aliyemkuta naye ambapo wanataka
afikishe miaka mitano ndipo wazae.
Post a Comment